Mbunge
wa Iringa Mjini anayemaliza muda wake Peter Msigwa, ameomba radhi kwa
kauli aliyowahi kuitoa katika uwanja wa Mwembe Togwa kuwa ‘Atakaye
muunga mkono Lowassa akapimwe akili’.
Akizungumza
kupitia kipindi cha Panga Pangua cha Azam TV, msigwa amesema ni kweli
yeye alitoa kauli hiyo lakini amedai naye ni binadamu na kuna wakati
anateleza.
“Ni
kweli na nimeipima akili yangu, nimechekecha, nikatafakari na mwisho wa
siku nikatambua kwamba kauli yangu niliitoa kimakosa.
Sasa hivi nathubutu kusema kuwa, Lowassa ndiye anfaa kuwa Rais wa Tanzania baada ya Dk Kikwete” alisema Msigwa.
Post a Comment