JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 16.10.2015.
· MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA MTOTO WAKE KUTOKANA NA MGOGORO WA KIFAMILIA.
· MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA JANGURUTU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MBARALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU
MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MWASHIWAWALA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA
DICKSON KAWAWA (50) ALIUAWA KWA KUPIGWA KWA VIPANDE VYA MATOFALI NA
MTOTO WAKE AITWAE SIKU DICKSON (20) MWENDESHA PIKIPIKI @ BODABODA,
MKAZI WA MWASHIWAWALA.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 15.10.2015 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA MWASHIWAWALA, KATA YA IWINDI, TARAFA YA USONGWE,
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA.
CHANZO
CHA KIFO HICHO NI KIPIGO NA KUTOKWA DAMU NYINGI BAADA YA MAREHEMU
KUKATAZWA NA MTOTO WAKE KUNYWA POMBE KWA MUDA MREFU NA KUKAIDI.
MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA UPELELEZI WA TUKIO HILI UNAENDELEA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU
MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA JANGURUTU WILAYA YA MBARALI AITWAYE JAILOS
GOYAGE (56) AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE
NAMBA ZA USAJILI T. 888 BRD AINA YA TOYOTA LAND CRUISER IKIENDESHWA NA
DEREVA AITWAYE OMARY NURU (36) MKAZI WA MPAKANI UBARUKU.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 15.10.2015 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO
KIJIJI CHA JANGURUTU, KATA NA TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA
WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA AMEKAMATWA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA WANAFAMILIA KUTATUA MIGOGORO YAO KWA KUKAA MEZA
YA MAZUNGUMZO. PIA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA
SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA
KUZINGATIA SHERIA/MICHORO NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA
AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment