JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 30.10.2015.
· WATU
WATATU WANAODHANIWA KUWA MAJAMBAZI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA.
· WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUMILIKI SILAHA KINYUME CHA SHERIA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
WATU
WATATU WANAODHANIWA KUWA NI MAJAMBAZI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.
KEFA ISRAEL MDEKWA (40) MKAZI WA MAKAMBAKO 2. EVARISTO MSEMWA (26) MKAZI
WA MAKAMBAKO NA 3. KIMESHU KITIPAI (36) MKAZI WA KIJIJI CHA MODELO
WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUMVAMIA MTU
MMOJA AITWAYE ASHERY MPANYAKAVI (32) MKAZI WA MKONDAMI WAKIWA NA SILAHA
KISU, PANGA/JAMBIA MBILI NA NONDO WAKIWA NA GARI YENYE NAMBA ZA
USAJILI T.278 BMJ AINA YA TOYOTA CHASSER.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 28.10.2015 MAJIRA YA SAA 23:50 USIKU HUKO
KATIKA KIJIJI CHA MKONDAMI, KATA YA MAWINDI, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA
MBARALI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, WATUHUMIWA HAO WALIMVAMIA MHANGA
AKIWA AMELALA NYUMBANI KWAKE NA ALIFANIKIWA KUPIGA KELELE ZA KUOMBA
MSAADA NDIPO WALIJITOKEZA WANANCHI NA KUMSAIDIA. MHANGA ALIJERUHIWA KWA
KUPIGWA NONDO MDOMONI HATA HIVYO ALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA.
HAKUNA MALI/KITU KILICHOCHUKULIWA KATIKA TUKIO HILO. UPELELEZI
UNAENDELEA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
WATU
WAWILI WAKAZI WA CHITETE WILAYA YA MOMBA WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA
YA SIMON BENARD (42) NA BONDIA PETER PANDISHA (38) WANASHIKILIWA NA
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA SILAHA/ BUNDUKI MBILI AINA YA
GOBOLE NA BASTOLA MOJA ILIYOTENGENEZWA KIENYEJI.
WATUHUMIWA
WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 29.10.2015 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI HUKO
KATIKA KIJIJI NA KATA YA CHITETE, TARAFA YA NDALAMBO, WILAYA YA MOMBA,
MKOA WA MBEYA. SILAHA HIZO ZILIPATIKANA BAADA YA KUFANYIKA UPEKUZI
KATIKA NYUMBA YA BONDIA PETER PANDISHA NA KUKUTWA ZIKIWA ZIMEFICHWA
KWENYE DARI LA NYUMBA. AIDHA INADAIWA KUWA, WATUHUMIWA HUZITUMIA SILAHA
HIZO KUFANYA UHALIFU.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTAFUTA KIPATO KWA NJIA HALALI NA
KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA UHALIFU KWANI VINA MADHARA KWA MAISHA YAO.
AIDHA
ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA
ZA MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO ILI UPELELEZI
UFANYIKE IKIWA NI PAMOJA NA KUWAKAMATA.
Imesainiwa na
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment