Tukiwa bado tupo kwenye headlines za Uchaguzi 2015 leo Octoba 7, 2015
Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva ametolea majibu
kuhusu Wanafunzi kushiriki Uchaguzi mkuu.
‘Suala la Wanafunzi mara kwa mara
limekuwa likiletwa na sisi kwenye tume tumesema kwamba linafanywa kama
la kisiasa kwa maana kwamba mara kadhaa wanafunzi walipokuja pale ofisi
za tume kile kikundi chao wakatuambia kwamba kipindi hiki watakuwa
likizo‘ Lubuva
‘Tukawapa ushauri na tukazungumza nao
nimeenda mpaka chuo cha Dodoma tukazungumza nao na tukawapa utaratibu
mpaka tukaunda kamati ikaongozwa na Jaji Mkwawa wasikilizwe wakaelezwa
na baadae wakaandikiwa barua kwa hiyo hili suala ni suala la kisiasa
na tumeshughulika nalo mwisho tukawaambia kwamba wamejinyima wenyewe
hii nafasi’- Lubuva
‘Kwa hiyo suala la wanafunzi ninasema
kwa niaba ya wenzangu kwamba kwenye tume tumefunga mlango na upande wa
kuboresha daftari umepita ni wao wenyewe wamejinyima na kuhusu kwamba
vyuo vifungwe kwasababu ya Uchaguzi Mkuu ni suala la Wizara ya Elimu
sio la tume ya Uchaguzi – Lubuva
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Jaji Damian Lubuva
Un
Post a Comment