………………………………………..
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) Jaji mstaafu Damian Lubuva ametoa ufafanuzi juu ya
ucheleweshaji wa matokeo ya awali ya ngazi Rais kutoka majimbo
mbalimbali nchini.
Akitangaza matokeo hayo katika
ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Oktoba 27, 2015 jijini Dar
es salaam Jaji Lubuva amesema kuwa Tume inasubiri matokeo hayo kutoka
kwa wasimamizi wa uchaguzi kutoka katika majimbo yote nchini.
“waandishi wa habari mnatakiwa
kuwa wavumilivu na kutangaza kile ambacho mnakisikia na si kupotosha
umma kwani Tume inatoa matokeo bila kupendelea chama chochote” aliongeza
Jaji Lubuva.Mbali na hayo jumla ya majimbo
87 yameshaleta majibu ya awali ya matokeo ya urais yakiwemo Mkoa wa
Kusini Pemba Jimbo la Nchonga ambapo jumla ya wananchi 8,018
walijiandikisha, 5949 walipiga kura na kura halali zilikuwa 5771 ambayo
ni asilimia 97.01 na 178.29 zilikataliwa.
Vilevile katika Jimbo la
Chunguni waliojiandikisha walikuwa 13,416 ambapo wananchi 10,108 sawa na
asilimia 75.34 walipiga kura, kura halali zilikuwa 9,792 sawa na
asilimia 96.92 pamoja na kura 311 zilikataliwa ambayo ni sawa na
asilimia 3.08.
Halikadhalika katika Mkoa wa
Mbeya Jimbo la Ileje jumla ya wananchi 56,002 walijiandikisha katika
daftari la kudumu la wapiga kura ambapo asilimia 78.56 sawa na 43,997
walipiga kura, kati ya idadi hiyo kura 43,098 zilikuwa halali na kura
896 sawa na asalimia 2.04 zilikataliwa.
Jaji Lubuva aliongeza kuwa
katika Jimbo la Ileje mkoani Mbeya ACT ilipata kura 501, ADC kura 347,
CCM kura 26,368, CHADEMA kura 15, 651, CHAUMA walipata kura 155, NRA
kura 26,TLP kura 36, pamoja na kura 20 kutoka chama cha UPDP.
Mbali na hayo majimbo mengine
yaliyowakilisha matokeo hayo ni pamoja an Jimbo la Mtama kutoka Mkoa wa
Lindi, Jimbo la Tunguu Mkoa wa kusini Unguja, Jimbo la kibaha Vijijini
Mkoa wa Pwani, Jimbo la Nachingwea, Jimbo la mtama kutoka mkoani Lindi,
Jimbo la Mafia mkoani Pwani pamoja Jimbo la Mkuranga mkoani Pwani.
Pia Mkoa wa Katavi Jimbo la
Mpanda vijijini, Mkoa wa Magharibi Mjini Jimbo la Fuoni, Jimbo la
Kikwajuni, Jimbo la Mwera, Jimbo la Amani na Jimbo la Magomeni Mkoa wa
Unguja Jimbo la Nungwi, Kaskazini Unguja Jimbo la Bumbwini, mkoa wa
Rukwa Jimbo la nkasi kusini, Mkoa wa Kagera Jimbo la Nkenge na Jimbo la
Byalamuro, kutoka Mkoani Arusha Jimbo la Arusha Mjini yaliwakilisha
matokeo yao.
Kwa upande wake Msaidizi wa
Mkurugenzi wa Uchaguzi Chadema Bwa. Matson Chizi amesema kuwa mchakato
mzima wa Uchaguzi ni mzuri wa wapo tayari kupokea matokeo hayo kwa jinsi
yatakavyokuwa.
Post a Comment