Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe
(kushoto), akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama ya Kisutu
Dar es Salaam leo.
Askari wa FFU wakiimarisha ulinzi mahakamani hapo.
Wafuasi wa Chadema wakionesha alama ya vidole viwili wanayoitumia.
Viongozi wa Chadema wakitoka katika mahakama hiyo baada ya kusikiliza kesi hiyo. |
Vijana waliokamatwa wakiwa katika mahakama hiyo.
Na Dotto Mwaibale
WATU
wanane akiwemo Raia mmoja wa Korea na raia mmoja wa Kenya wamepandishwa
kizimbani kwa kusambaza taarifa za matokeo ya urais katika Mtandao wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi yakiwa na kichwa 'M4C election result
management system' bila kuthibitishwa kwa lengo la kupotosha umma.
Sanjari
na hilo, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), amewasilisha mahakamani
hati ya kuzuia dhamana ya washtakiwa kwa kile alichadai kuwa ni kwa
sababu ya usalama na kwa maslahi ya Taifa.
Washtakiwa
hao ni Mashinda Mtei (49) mkazi wa Tengeru Arusha, Julius Mwita (40)
mwanasiasa na ni mkazi wa Magomeni, Frederick Fussi (25) IT, mkazi wa
Mbezi, Julius Matei (45) raia wa Kenya, Meshack Mlawa (25) mchungaji na
ni mkazi wa Keko, Anisa Rulanyan (41) Mhandisi, mkazi wa Kawe, Jose Nimi
(51) mkazi wa Uingereza na Kim Hyunwook (42) raia wa Korea.
Wakili
wa Serikali Mkuu Edwin Kakolaki alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi
Respicius Mwaijage wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam
kuwa washtakiwa wanashtakiwa kwa mashtaka matatu.
Ilidaiwa
kuwa katika shtaka la kwanza linawakabili washtakiwa wote, ambapo
inadawa kati ya Oktoba 25 na 26 mwaka huu, wakiwa katika vituo tofauti
tofauti ndani ya jiji la Dar es Salaam walitoa taarifa za uongo kwenye
mitandao wakati wakijua hazijadhibitishwa.
Kakolaki
alidai washtakiwa hao walisambaza taarifa hizo kwenye mtandao huo na
katika mitandao mingine ya kijamii ambayo ni Facebook na Twitter
kutangaza matokeo ya urais ya mwaka huku kwa lengo la kuposha umma huku
wakijua hayajadhibitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Katika
shtaka la pili linamkabili Matei, Nimi na Hyunwook, ambapo wanashtakiwa
kuwa Oktoba 26 mwaka huu wakiwa katika hoteli ya King iliyopo Kinondoni
, Dar es Salaam wakiwa na hati za kusafirilia zenye namba A1532119,
930879 na M 27687807 walijiingiza katika ajira ya kukusanya na kusambaza
matokeo ya urais ya uchaguzi wa mwaka huu ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema ) bila kibali.
Pia,
alidai katika shtaka la tatu lina mkabili Matei peke yake ambaye akiwa
raia wa Kenya mwenye hati ya kusafirilia namba A1532119 akiwa ndani ya
jiji la Dar es Salaam alijihusisha na biashara katika Saccos ya Wanama
bila kibali.
Baada
ya washtakiwa hao kusomewa mashtaka hayo, walikana kuhusika na tuhuma
hizo, ambapo Kakolaki alidai upelelezi bado haujakamilika na pia alidai
DPP amewasilisha hati ya kuzuia dhamana kwa sababu ya usalama na maslahi
ya Serikali.
Wakili
wa washtakiwa hao Peter Kibatala, alidai kuwa mashtaka yanayowakabili
wateja wake yanadhaminika, kwa hiyo aliiomba mahakama iwapatie dhamana.
Pia,
alidai hati hiyo ya DPP haiko mahakamani hapo kihali na kuiomba Mahakama
itupilie mbali hati hiyo kwa sababu haina mashiko kisheria.
Kibatala
alidai kuwa hati ya mashtaka iko tofauti na hati ya DPP kutokana na
kifungu kilichokuwepo kuwa si sahihi, kwa hiyo kama ni hivyo hati hizo
zote hazifai, kutokana na mapungufu hayo.
Baada
ya Kibatala kudai hivyo, wakili Kakolaki alidai kuwa hati ya DPP ipo
kihalali mahakamani na anayuetakiwa kuthibitisha hilo na mahakama kwa
hiyo waiyachie mahakama.
Alidai
kuhusu kifungu kilichotumika ni sahihi, akaiomba mahakama itupilie
mbali hoja za Kibatala na washtakiwa wanyimwe dhamana kwa mujibu wa
sheria, baada ya DPP kuwasilisha hati hiyo.
Hakimu Mwaijage alisema uamuzi wa hoja hizo atazitoa Oktoba 30 mwaka huu na washtakiwa aliamuru warudishwe rumande.
Nje ya mahakama
Washtakiwa
hao waliondoka katika eneo hilo la mahakama wakiwa chini ya ulinzi
mkali wa Jeshi la Polisi ambapo wakiwa ndani ya magari ya polisi
walikuwa wakionesha alama za vidole viwili.
Mwenyekiti
wa Chadema Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salim
Mwalimu, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sauti, Profesa Mwasiga Baregu na
viongozi wengine wa Chadema walijitokeza mahakamani hapo kufuatilia
shauri hilo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com.
Post a Comment