Aliyekuwa
mgombea wa Urais, Anna Mgwira akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na mwenendo wa siasa ulivyofanyika hapa nchini pamoja na
kuwashukuru baadhi ya waandishi wa habari kwa kuripoti habari
waliojitokeza katika kampeni bila kujari itikadi zao katika mkutano wa
waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwao jijini Dar es Salaam.
Mbunge
wa Jimbo la Kigoma Mjini kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo, Zitto
Kabwe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
kuhusiana na kushinda kwa chama chake katika jimbo la Kigoma Mjini
pamoja na Kuongoza kupata madiwani katika kata 50 hapa nchini na katika Manispaa ya Kigoma Ujiji kufanikiwa kuunda baraza la madiwani ikiwa Manispaa hiyo ina kata 18 chama cha ACT-Wazalendo kushinda na kupata madiwani 12 na CCM ikipata kata 5 na Chadema kata 1 ikiwa kata moja haikufanya uchaguzi na itafanya Jumapili Ijayo.
Kutoka
kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha ACT -Wazalendo, Samson Mwigamba
katikati ni aliyekuwa mgombea wa Urais wa chama cha ACT-Wazalendo,Anna Mgwira na kulia ni Mbunge
wa Jimbo la Kigoma Mjini kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo, Zitto
Kabwe wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
leo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhulia katika mkutano na viongozi wa chama cha ACT-Wazalendo jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
CHAMA
Chama cha ACT Wazalendo kimemwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, John Magufuli ahakikishe Tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC)
itangaze matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu ili
walioshinda watangazwe na waapishwe kwaajili ya kuanza kazi katika
serikali ya Zanzibar ikiwa mpaka sasa Zanzibar haina Serikali.
Zitto amesema kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) hakuwa
na mamlaka yoyote ile katika tume hiyo ya kukufuta matokeo ya uchaguzi
Zanzibar kwani tume inawajumbe wake yeye peke yake hana mamlaka hayo.
Pia zitto amesema kuwa chama chake kitafanya kazi kwaajili ya masrahi ya wananchi ya sasa na yabaadae, pia amesema kuwa chama chake hakitashiriki katika kugombea nafasi ya spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Post a Comment