Dereva wa gari hili Z 511 FG
ambaye inaaminika ni askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
(TPDF) (jina halikupatikana) ameponea chupuchupu baada ya mifumo ya usalama ya
gari hili ilipofanikiwa kufyatua puto mara tu baada ya gari hili kukosa
mwelekeo na kugonga mnazi.
Ajali hii imetokea katika kijiji cha Kibele, Wilaya ya Kati
Mkoa wa Kusini Unguja na inaaminika kuwa dereva huyo alishindwa kuidhibiti gari
ndogo aina
ya Toyota Spacio kutokana na mwendo kasi ambayo ilihama barabarani na kugonga mnazi ambao uliangukia gari na baadae gari kuwaka moto.
ya Toyota Spacio kutokana na mwendo kasi ambayo ilihama barabarani na kugonga mnazi ambao uliangukia gari na baadae gari kuwaka moto.
Dereva alitolewa ndani ya gari akiwa amebanwa na puto (air
bags) zilizofyatuka na kuokoa uhai wake.
Alipata majeraha madogo ya kuchubuka kwenye mikono yake iliyokuwa inavuja damu.
Post a Comment