Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ALIYETOA SIRI ZA MUHIMBILI APATWA NA MAKUBWA



ChachaChacha Makenge akiugulia.
Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
CHACHA Makenge 38, (pichani), mgonjwa aliyetoa siri na malalamiko yake kwa Rais Dk. John Magufuli ‘JPM’ kuhusu ukosefu wa mashine ya kutambua magonjwa mbalimbali ya binadamu kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) yamemkuta makubwa baada ya watu wasiojulikana kuingia kwenye makazi yake maeneo ya Chuo Kikuu cha Mlimani jijini Dar na kumwibia kila kitu.

DK-MAGUFULIRais Dk. John Magufuli alipotembelea Hospitali ya Taifa, Muhimbili.
JIRANI AMJULISHA
Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa bado wodini na ni siku moja baada ya Rais Magufuli kutembelea Muhimbili, Makenge alisema siku hiyo kuna jirani yake alikwenda kumjulia hali, akamwambia nguo zake, vyombo na nyaraka mbalimbali vimeibwa na watu wasiojulikana.
Makenge aliongeza kuwa, taarifa za kuibwa kwa vitu hivyo zilimsononesha sana hasa akizingatia kuwa, maisha yake hayana adui na mtu na hajui aliyeiba ana lengo gani.
“Kule kwenye makazi yangu naishi peke yangu, sina uadui na mtu. Nilipopatwa na matatizo ya kupigwa hadi kuvunjwa mgongo na wanajeshi, nilipelekwa Hospitali ya Palestina, Sinza (Dar) na hali yangu ilikuwa mbaya, nikakimbizwa hapa Muhimbili kwa matibabu zaidi huku nikiambiwa kwenye makazi yangu kutakuwa salama,” alisema Makenge.
ANA WASIWASI NA NANI?
Gazeti hili lilimuuliza Makenge kama ana wasiwasi na mtu yeyote ambapo alisema:
“Kama wasiwasi kibinadamu lazima uwepo. Lakini simtaji mtu yeyote. Ila wasiwasi wangu mwingine ni usalama wa maisha yangu. Nahofia sana nikirudi. Maana najiuliza je hao watu wangenikuta wangeniacha kweli?
NYARAKA ZA NINI?
Alipoulizwa kuhusu nyaraka zilizoibwa kama kuna kitu cha siri, alijibu: “Ni mambo yangu mwenyewe. Kila mtu ana mambo yake ya siri ambayo hapendi mwingine ajue. Ila kwa mtu mwingine hawezi kuambulia kitu kwenye nyaraka kwani, najua mwenyewe nilivyokuwa naandika.”
ALIOMBA DAKIKA TANO KWA MAGUFULI
Makenge amekaa Muhimbili kwa miezi miwili bila matibabu kutokana na mashine ya CT Scan na MRI kwenye hospitali hiyo kuharibika na fedha kwa ajili ya vipimo katika hospitali binafsi hana lakini Rais Magufuli alipotembelea hospitali hiyo kwa kushtukiza Novemba 9, mwaka huu, mgonjwa huyo alimwomba dakika tano tu ili atoe yake ya moyoni.
ALICHOMWAMBIA RAIS
Mgonjwa huyo alipopewa muda huo, alimweleza rais kuhusu tatizo la kuharibika kwa mashine hizo na kumfanya yeye kulazwa hapo kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja bila matumaini na hakuwa na pesa za kwenda kupimwa na mashine za hospitali binafsi.
Ndipo Rais Magufuli alipouagiza uongozi wa Muhimbili kuhakikisha kuwa Makenge anapata vipimo hata nje ya hospitali hiyo na kutibiwa haraka, ikibidi atatoa mshahara wake utumike kumtibu.
Pia Magufuli aliagiza ndani ya wiki moja, na si zaidi ya wiki mbili, mashine za T Scan na MRI ziwe zimetengenezwa. Hadi tunakwenda mitamboni mashine ya MRI ilikuwa imeshaanza kufanya kazi baada ya matengenezo.
Kufuatia amri hiyo ya rais, Makenge alisema siku iliyofuata alipelekwa Hospitali ya Besta iliyopo  jijini Dar na kupimwa na kipimo cha MRI.
“Nilifanyiwa vipimo Novemba 10, mwaka huu, saa 4.13 asubuhi, alinipeleka muuguzi aitwaye Dora kwa kutumia gari la kubebea wagonjwa. Novemba 11, mwaka huu nilirudishwa hapa Muhimbili.
“Nilichukuliwa vipimo vya damu saa 5.18, baadaye akaja Dk. Antony, bingwa wa uti wa mgongo, kisha baadaye Dk. Frank na wenzake wakaja wakasoma majibu ya kipimo cha damu na MRI.
“Waliniambia kipimo cha MRI kitarudiwa na nitafanyiwa hapahapa Muhimbili, Jumanne ijayo (leo) kwani mashine imeshatengenezwa,” alisema mgonjwa huyo ambaye hawezi kutembea.
TUJIKUMBUSHE KWA RAIS MAGUFUILI
Baada ya maelezo ya Makenge, Rais Magufuli alizungumza na kiongozi mmoja wa hospitali hiyo ambapo naye alikiri kuharibika kwa mashine hizo. Rais alionekana kushtuka na kuumizwa na hali hiyo, akasema:
“Tatizo la hospitali za serikali mnaharibu vifaa ili vikafanye kazi kwa watu binafsi, vifaa vya hospitali za private (binafsi) zinafanya kazi lakini za hapa Muhimbili hazifanyi kazi…! Na watu wanasafiri kwenda Ulaya… Mungu atawalipa.”
KUHUSU MAKENGE
“Mpelekeni huyu mgonjwa (Makenge) akafanyiwe matibabu na mimi nitatoa hata mshahara wangu kumlipia, haiwezekani akakaa mwezi mzima..! Na nitalifuatilia.”

GPL
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top