Mshambuliaji
wa Azam FC, Didier Kavumbagu akitafuta mbinu za kumtoka veki wa Toto
African, Hamis Seleman katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara
uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. (Picha na
Francis Dande)
Beki wa Toto African, Salum Chuku (katikati) akichuana na
mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbagu (wa pili kushoto) wakati wa mchezo wa
Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar
es Salaam jana. Azam ilishinda 5-0.
Kipre Tchetche akimiliki mpira huku beki wa Toto African akijaribu kumzuia.
Wachezaji wa Azam FC wakishangilia baada ya kupata bao.
Kocha
Mkuu wa Toto African, Martin Grelics (kulia) akiwa katika picha ya
pamoja na kikosi cha kwanza cha timu hiyo kilichoanza kucheza na Azam FC
kwenye Uwanja wa Chamazi. Kocha huyo amevunja mkataba na kuwaaga
wachezaji wa timu hiyo.
Wachezaji wa Toto African wakiwa wamebeba ujumbe uliokuwa unasomeka 'Asante Sana Kocha Martin'
Kocha
Mkuu wa Toto African, Martin Grelics akiagana na wachezaji wake baada ya mchezo na Azam FC
kwenye Uwanja wa Chamazi. Kocha amevunja mkataba na timu hiyo.
Wachezaji wa Toto African wakiomba dua katika mchezo wao dhidi ya Azam FC.
credit: Michuzi-matukio blog
Post a Comment