BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
AWAMU YA PILI YA WANAFUNZI WALIOPANGIWA MIKOPO KWA 2015/2016
BODI
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuutaarifu umma kuwa
kuna taarifa zinazosambazwa na baadhi ya mitandao ya kijamii kuwa Bodi
haitatoa mikopo kwa waombaji wapya kwa mwaka wa masomo 2015/2016.
Taarifa hizo si za kweli na hivyo Bodi inauomba umma kuzipuuza.
Aidha,
Bodi ya Mikopo inapenda kutoa taarifa kwamba hadi sasa
imekwishawapangia mikopo jumla ya waombaji mikopo wenye sifa 40,836 wa
mwaka wa kwanza. Katika awamu ya kwanza, Bodi ilitoa orodha yenye jumla
ya waombaji 12,282 waliofanikiwa kupata mikopo na katika Awamu ya Pili
iliyotolewa tarehe 9 Novemba, 2015 jumla ya waombaji 28,554 wamepangiwa
mikopo.
Majina
ya waombaji waliofanikiwa kupata mikopo kutoka katika awamu zote mbili
yanapatikana kupitia mtandao wa Bodi wa olas.heslb.go.tz na tovuti ya
Bodi (www.heslb.go.tz). Aidha, orodha hizo pia zimetumwa vyuoni kwa
ajili ya taratibu za usajili.
Lengo
la Bodi ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wenye sifa
kupata mikopo katika mwaka wa masomo 2015/2016, ambao ni 50,830,
wanapata mikopo.
Aidha,
Bodi inapenda kuwasihi waombaji wa mikopo kuwa watulivu wakati mchakato
wa upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wenye sifa unaendelea.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Post a Comment