Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Bugando yalaani polisi kupiga mabomu ya machozi hospitalini

Uongozi wa hospitali ya rufaa Bugando jijini Mwanza, umelaani matumizi mabaya ya mabomu ya machozi yaliyofanywa na jeshi la polisi mkoani Mwanza kwa lengo la kuwatawanya wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo ( Chadema ) ndani ya hospitali hiyo na kusababisha taharuki kubwa kwa baadhi ya wagonjwa pamoja na watumishi wa hospitali hiyo.

Mkurugenzi mkuu wa hospitali hiyo Prof. Kien Mteta amesema kitendo cha jeshi la polisi kufyatua mabomu ya machozi katika eneo la chumba cha kuhifadhia maiti kimewatia hofu wagonjwa na wauguzi na kuongeza kuwa amesikitishwa kuona ugomvi wa kisiasa ukihamia ndani ya hospitali hiyo na kwamba tayari ameijulisha wizara ya afya na ustawi wa jamii kuhusu kadhia hiyo pamoja na kuliwasilisha kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza ambao wamezungumza kuhusu hatua ya jeshi la polisi kutumia mabomu ya machozi ndani ya hospitali hiyo inayomilikiwa na kanisa katoliki, wameeleza kushangazwa na tukio hilo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, naibu kamishna Charles Mkumbo anasema askari polisi hawakuwa na namna nyingine ya kumuokoa askari mwenzao, mkaguzi msaidizi wa polisi wilayani Geita Ngasa Joseph, zaidi ya kuwatawanya wafuasi wa Chadema kwa mabomu wakati walipokuwa wakimshambulia na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili wake.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top