Jaji
wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Lameck Mlacha, ametupilia mbali
mapingamizi yaliowekwa na RPC wa Mwanza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali
kuwa mleta maombi ambae ni Baba mdogo wa Mawazo hana uhalali wa kisheria
wa kuleta maombi hayo kwa kuwa yeye si baba mzazi wa marehemu, na kuwa
hajaleta hoja za kubishaniwa kwenye maombi hayo.
Upande wa utetezi unaoongozwa na mawakili John Mallya, James Millya na Paul Kipeja ulijibu hoja hizo kuwa katika hatua hiyo masuala ya kubishaniwa hayana sababu ya kuletwa kwa kuwa ni hatua ya awali sana.
Kuhusu uhalali wa kisheria wa baba mdogo wa marehemu, majibu yalikuwa
kwamba baba mdogo kwa kuwa ndiye aliemlea Marehemu Mawazo, anayo mamlaka
na uhalali wa kisheria wa kuleta maombi hayo.
Mahakama imekubaliana na hoja za mawakili wa mleta maombi na kuamua
kuruhusu kesi ya msingi kufunguliwa kama ilivyoombwa, na kutupilia mbali
mapingamizi ya RPC na AG.
Upande wa wapeleka maombi utawasilisha maombi ya kesi ya msingi leo hii
mchana, kisha tutasubiri maelekezo ya Mahakama kuwa kesi hiyo itaanza
kusikilizwa lini!
Post a Comment