Kalenda
ya dirisha la usajili kwa vilabu vya Ligi Kuu (VPL), Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) lilofunguliwa Novemba 15,
litafungwa Disemba 15 mwaka huu.
Vilabu
vinavyoshiriki ligi hizo zilizopo chini ya Shirikisho Mpira wa Miguu
(TFF) vinaombwa kufanya usajili katika muda uliopangwa ili kuepukana na
kuchelewa, na kufungwa kwa dirisha hilo.
Usajili
wa dirisha dogo ni kwa vilabu ambavyo havijajaza idadi ya wachezaji 30
katika usajili uliofanyika wakati wa dirisha kubwa la usajili (Juni –
Agosti 2015), usajili huo wa wachezaji unafanyika katika tovuti ya TFF, www.tff.or.tz kisha kwenye link ya Club Registration.
Post a Comment