Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Dkt. Magufuli Alivyoapishwa Rasmi Kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri Ya Muungano Tanzania .... Hizi hapa picha 300 za tukio zima




Wananchi wenye shauku ya kuona tukio la kuapishwa kwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, Dk. John Magufuli na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, wakiwa wamepanga foleni kuingia katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo asubuhi
Wananchi wakiwa wamejikinga mvua kwa mwavuli wakati mvua ilipokuwa ikinyesha kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, wakati wa tukio la kuapsihwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, Dk. John Magufuli na Makamu wa Rais Mama samia Suluhu Hassan leo
Mwananchi akijikinga muavuli na mwaae wakati mvua ilipokuwa ikinyesha kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, wakati wa tukio la kuapsihwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, Dk. John Magufuli na Makamu wa Rais Mama samia Suluhu Hassan leo
Hali ya eneo la kuapishia lilivyokuwa kabla ya tukio la  tukio la kuapsihwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, Dk. John Magufuli na Makamu wa Rais Mama samia Suluhu Hassan leo
Baadhi ya viongozi wa dini na watu mashuhuri, wakiwa kwenye hema maalum wakati wa tukio la kuapsihwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, Dk. John Magufuli na Makamu wa Rais Mama samia Suluhu Hassan leo
Baadhi ya viongozi na wageni waalikwa wakiwsili katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, wakati wa tukio la kuapsihwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, Dk. John Magufuli na Makamu wa Rais Mama samia Suluhu Hassan leo
Viongozi wa dini wakienda jukwaa la kuapishia wakati wa tukio la kuapsihwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, Dk. John Magufuli na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan leo
Maadamano kuelekea eneo la kuapisha, yalianza kwa kuongozwa na jaji Mkuu wa Tanzania, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, wakati wa tukio la kuapsihwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, Dk. John Magufuli na Makamu wa Rais Mama samia Suluhu Hassan leo
Jaji Mkuu wa Tanzania na Spika wa Bunge wakipanda jukwaani
Makamu wa Rais Mstaafu, Dk. Mohammed Gharib Bilal na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein wakienda kwenye eneo la kuapisha wakati wa tukio la kuapsihwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, Dk. John Magufuli na Makamu wa Rais Mama samia Suluhu Hassan leo
Rais wa awamu ya tano Dk. John Magufuli akienda eneo la kuapishiwa huku akiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick
Rais Dk. Magufuli akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohammed Othman Chande kabla ya kuapishwa
Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akiwasili Uwanjani
Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akiwasili Uwanjani
Rais staafu Jakaya Kikwete akienda kukagua gwaride rasmi la kumuaga
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete baada ya kukagua gwaride rasmi
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete baada ya kukagua gwaride la Omega
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipigiwa mizinga na wimbo wa Taifa
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete baada ya kupigiwa mizinga na wimbo wa taifa
Rais mstaafu Jakaya Kikwete akienda eneo la kuapishiwa Rais mpya Dk. Magufuli
Rais wa awamu ya Tao Dk. John Magufuli akiapishwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo
Rais wa awamu ya tano John Magufuli akitia saini kiapo chake
Rais wa awamu ya tano Dk. John Magufuli akikabidhiwa kiapo chake baada ya kusaini na Jaji Mkuu
Jaji Mkuu akimpongeza Rais John Magufuli baada ya kumuapisha
Rais Dk. John Magufuli akikabidhiwa mkuki ikiwa ni ishara ya kupokea ukumbwa
Dk. Magufuli akionyesha mkuki na ngao baada ya kukabidhiwa
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiapa mbele ya Jaji Mkuu
Mama Samia akisaini kiapo
Jaji Mkuu akimkabidhi Mama Samia kiapo chake baada ya kusaini
Kisha akampongeza
Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, Dk. John Maguli  na Makamu wake wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan wakiwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na makamu wa Rais Mstaafu Dk. Bilal, baada ya kuapishwa.
Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, Dk. John Maguli  na Makamu wake wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan wakiwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na makamu wa Rais Mstaafu Dk. Bilal, baada ya kuapishwa.
Sheik Mkuu Mufti wa Tanzania Abubakary Zuberi akisoma dua baada ya Dk. Magufuli na mama Samia kuapishwa
Kardinali Polycarp Pengo akiomba dua baada ya Dk. Magufuli na Mama Samia kuapishwa

Rais Mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete na makamu wake Mstaafu Dk. Mohammed Gharib Bilal wakitoka eneo la kuapishia na kwenda jukwaa la juu, baada ya Dk. Magufuli na Mama Samia kuapishwa
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Dk. Bilal wakiwa kwenye gari maalum wakati wakienda jukwaa juu, huku wakionekana wenye furaha
Mama Samia akitoka jukwaani
Vongozi wa dini wakitoka jukwaa la kuapishia
Rais wa awamu ya tano Dk. Magufuli akiwa amebaki na Mkuu wa JJeshi la Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kwenye jukwaa la kuapishiwa
Rais wa awamu ya tano Dk. John Magufuli akipigiwa mizinga na wimbo wa taifa baada ya kuapishwa

Dk. Magufuli akikagua gwaride la Alfa la Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania kuashiria kuanza utawala wa Urais awamu ya tano
Baadhi ya waliohudhuria hafla hiyo
Baadhi ya waalikwa
Rais Magfuli akienda jukwaa kuu kuungana na viongozi mbalimbali
Viongozi mbalimbali akiwemo Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na wale wa kutoka nchi za nje wakisimama kumlaki Rais Magufuli jukwaa kuu
Rais Dk. Magufuli akiwasalimia wageni wakati akipanda kwenda jukwaa kuu
Rais Dk. Magufuli akisalimiana na Mkewe Mama Janet
Rais John Magufuli akikumbatiwa kwa Rahaaa, na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete
"Kiti chako hicho hapo Mzee", Ni kama Rais mstaafu Kikwete alikuwa akisema hivyo kumwambia Rais Magufuli alipowasili jukwaa kuu
Rais Magufuli na Rais Mstaafu Kikwete wakiteta jambo
Rais Magufuli akipokea salam za heshima kutoka kwenye gwari
"HIMA HIMAAAA.. TANZANIAAAA", Wanajeshi wa JWTZ wakipaza sauti wakati wakitoa salam ya Rais kwa Dk. Magufuli

Ndege Vita zikipita Uwanja wa Uhuru kutoa salamu kwa Rais mpya, Dk. agufuli
Licha ya Uwanja wa Uhuru kufuria wananchi lakini mamia wengine walilazimika kubaki nje, baada ya uwanja huo kujaa. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO


Hatimaye, Dkt. John Magufuli ameapishwa rasmi na kuwa Rais wa serikali ya awamu ya Tano ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania akihitimisha rasmi uongozi wa serikali ya awamu ya nne iliyoongozwa na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.
 
Rais Magufuli na makamu wake Bi. Samia Suluhu wamekula kiapo leo katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mbele ya viongozi wa nchi mbalimbali pamoja na viongozi wa chama, serikali na viongozi wa dini ambazo zilinogeshwa zaidi na gwaride la Jeshi la Wananchi.

Dkt. Magufuli ameapishwa na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Othman Chande na kupigiwa mizinga 21 ya heshima baada ya kukabidhiwa kijiti cha uongozi na rais wa serikali ya awamu ya nne, Jakaya Kikwete.

Katika Jukwaa la Kiapo, walikuwepo Jaji Mkuu, Othman Chande, Katibu Mkuu Balozi Ombeni Sefue pamoja na Spika wa Bunge la 10, Bi. Anne Makinda na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
 
Wengine waliokuwa katika jukwaa la Kiapo ni pamoja na Rais wa serikali ya awamu ya nne, Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa serikali ya awamu ya nne, Dkt. Gharib Ali Bilal, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Ali Shein.
 
Rais wa awamu ya nne, alipigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride maalum la jeshi la Wananchi kama  ishara ya kumuaga kwa heshima na kuteremsha bendera yake, kabla hajakabidhi madaraka kwa rais mpya Dkt. Magufuli.
 
Pia, viongozi wa dini za aina Tatu walihusika katika kuunda jopo la kiapo na kutoa sala zao kuliombea Taifa na Rais Mpya, Dkt. John Magufuli.
 
Marais wa nchi mbalimbali waliohudhuria ni pamoja na Paul Kagame (Rwanda), Jacob Zuma (Afrika Kusini), Robert Mugabe (Zimbabwe), Uhuru Kenyatta (Kenya), Yoel Museven (Uganda), Rais wa Msumbiji pamoja na mawaziri wa nchi mbalimbali.
 
Sherehe hizo zilihudhuriwa na maelfu ya wananchi na kupata baraka ya mvua wakati wote lakini wananchi hao waliendelea kufuatilia tukio hilo la kihistoria.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top