DIAMOND PLATNUMZ
Jina
lake kamili ni Nassib Abdul, huyu wengi wamempachika jina la sukari ya
warembo, idadi kubwa ya wanawake wanampenda kutokana na mwonekano wake
na pia uwezo wake mkubwa wa kucheza na sauti anapoimba ingawa wengi
hudai hana sauti nzuri lakini huvutiwa na namna anavyoweza kuitumia
sauti hiyo na kuwa kivutio katika nyimbo zake.
Maonyesho yake hujaza watu wengi lakini inakadiriwa wasichana wengi
hujitokeza katika matamasha ambayo hutangazwa kwamba msanii huyu
atakuwepo, pia wengi wao hutamani kumshika msanii huyu ndiyo maana wengi
wao hukimbilia kumtunza.
ALI KIBA
Msanii
huyu anayetamba na wimbo wa ‘Mwana Dar’ na ‘Chekecha Cheketua’ jina
lake kamili ni Ally Salehe Kiba, licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kuimba
na kucheza lakini wanawake wengi huvutiwa na uwezo wake wa kuchezea
sauti yake katika kuimba na pia mwonekano wake akiwa jukwaani ndiyo
maana mashabiki wake huwa wakimshangilia kwa sauti na kelele zote
wapendavyo kila anapokuwa jukwaani.
CHRISTIAN BELLA
Huyu
ni zaidi ya msanii kutokana na kuwa na kipaji kikubwa katika sanaa yake
ya muziki, wanawake huvutiwa naye kwa sauti yake yenye mvuto wa hali ya
juu na namna anavyojiweka akiwa jukwaani na pia ana uwezo mkubwa wa
kucheza na mashabiki wake kiasi cha kuteka hisia za mashabiki wake.
Wanawake pia huvutiwa naye kiasi kwamba wengine humtaka zaidi ya muziki
na jambo hilo alishakiri mwenyewe kwamba wapo mashabiki wake wanaomsaka
kwa ajili ya kupata penzi lake.
YAMOTO BAND
Wasanii
hawa kwa ujumla wao wamekuwa kivutio kikubwa kwa wanawake hasa wawapo
jukwaani, wengi wao wameonekana kutamani kujumuika na kucheza nao
jukwaani lakini wanaposhindwa wasanii hao hushuka jukwaani na
kujichanganya nao hasa mashabiki wao wa kike.
Mara kadhaa wasanii wanaounda kundi hilo walishawahi kueleza kwamba wapo
wanawake watu wazima huwafuatilia kwa kutaka kuwapongeza zaidi ya
wanavyoimba jukwaani.
DIMPOZI KWA POZI
Anafahamika
kama Ommy Dimpoz lakini jina lake kamili ni Omary Faraji Nyembo,
wanawake huvutiwa zaidi na msanii huyu kutokana na nyimbo zake za
kimapenzi ndiyo maana kila anapokuwa jukwaani humpigia kelele za
kutosha.
MR BLUE
Msanii
huyu ni wa muda mrefu asiyechuja, alipata umaarufu kwa jina la Mr Blue
jina lake kamili ni Herry Sameer, ndiye msanii pekee wa hip hop
anayewavutia zaidi wasichana kutokana na nyimbo zake kuwa na vionjo vya
kimapenzi ambayo huwagusa zaidi wasichana.
BARNABA
Anaitwa
Elias Barnaba, ni mmoja wa wasanii wasiobadili majina yao ya kisanii,
uzuri wa sauti yake na uwezo wake wa kuimba jukwaaani na kutumia vyombo
mbalimbali vya muziki ndiyo silaha yake kubwa kuwa kivutio kwa wanawake.
Mwenyewe hupenda kujiita kipenzi cha mabinti kutokana na kwamba wanawake
wengi huziimba nyimbo zake mwanzo mwisho, pia ndiye msanii aliyeimba
kwa ushirikiano mkubwa na wasanii wa kike ndani na nje ya nchi ambapo
kwa sasa yupo mbioni kurekodi wimbo wa kushirikiana na msanii wa kike
kutoka nchini Nigeria.
BOB JUNIOR
Ray
C alifahamika kama kiuno bila mfupa na Raheem Rummy Nanji maarufu Bob
Junior naye hivyo hivyo, wasichana wengi huvutiwa na kiuno chake
anapocheza jukwaani, katika maonyesho yake mengi wasichana wameonekana
kujaa kutokana na kuwa na mvuto naye kwa namna anavyovaa, anavyomiliki
jukwaa na namna nyingine nyingi wanazovutiwa kwake.
JUX
Huyu
ndiye mpenzi wa msanii maarufu, Vanessa Mdee, Juma Jux licha ya
kuchipukia katika muziki wa Bongo Fleva lakini juhudi zake na uwezo wake
wa kuchezea sauti yake, aina ya mavazi, namna anavyojiweka vimekuwa
mvuto mkubwa kwa wasichana kiasi kwamba wengi wao hujikuta wakipiga
kelele za kutosha katika maonyesho yake.
Ben Pol.
Sophia
ngoma ambayo inahit hadi sasa kutoka kwa msanii Ben Pol wadada kwa
wakaka wakiusikia basi inakuwa shida mpya ndani ya miyo. Msanii huyu
anaongoza kwa sauti ya pekee kwenye uimbaji wa Rn'B hapa Bongo.
chanzo;the choice
Post a Comment