Wasanii
wa filamu za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’ na Steve Nyerere wikiendi
iliyopita inasemekana walikula chakula chenye sumu,ambapo mpaka sasa
Steve Nyerere bado amelazwa hospitali.
JB amezungumza na 255 kupitia XXL na kusema hivi:
‘’Siku
ya Ijumaa tulikula kitimoto na vyakula tofauti tofauti sasa asubuhi
yake ndio tumbo likaanza kuniuma niliendesha sana nikaenda hospitali
nikapewa dawa nilivyokunywa hazikunisaidia usiku wake tumbo likaniuma
sijawahi kuumwa tumbo kama nilivyoumwa siku ile hata kuongea sikuweza
nikapigwa sindano mbili moja ya mshipa na nyingine ya nikapewa vidonge
viwili daktari akaniambia nipumzike’’Alisema JB .
‘’Siwezi
kusema kama inahusiana na ishu ya uchaguzi ninachosema ni kuwa chakula
kilijuwa sio kizuri,tulikula wote kitimoto na kuanzia leo nimekoma kula
kitimoto na pamoja na kulakula ovyo,nilienda hospitali kupima daktari
akaniambia nimekula chakula kibovu ukweli ni kwamba niliumwa tumbo sana
siku ile’’alisema JB.
Post a Comment