Baada ya kuteuliwa na CCM na kupita katika mchakato wa kumpata mgombea Uspika wa Bunge la Kumi na moja bila kupingwa, Job Ndugai ameeleza changamoto anazotarajia kukutana nazo ikiwa ni pamoja na migomo.
Akiongea
na waandishi wa habari jana baada ya jina lake kupitishwa, Ndugai
alilielezea Bunge la kumi na moja kama Bunge lenye utofauti mkubwa na
mabunge mengine huku akidai kuwa ongozeko la vijana wengi na wasomi
wengi zaidi kunaashiria kuongezeka kwa changamoto zaidi.
“Bunge
hili lina wabunge wengi vijana, lina wabunge wengi wasomi zaidi kuliko
mabunge yote yaliyowahi kutokea na lina uwakilishi mkubwa. Hili ni Bunge
ambalo litakuwa na changamoto nyingi, tetegemee migomo ya hapa na pale,
hata hivyo ubora wa kazi utakuwa mkubwa,” alisema Ndugai.
Hata
hivyo, Ndugai alisisisitiza kuwa ataliongoza Bunge kwa weledi na
kutenda haki kwa kila upande hivyo aliwataka wabunge wote wakiwemo wa
upinzani kumuunga mkono leo ili awe Spika wa Bunge la 11.
Post a Comment