JUKWAA la Wahariri (TEF), limelaani kitendo cha kuzomewa na kudhalilishwa kwa waandishi wa habari wa ITV, katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam, Oktoba 30 mwaka huu.
Akizungunza
na waandishi wa habari Katibu wa Jukwaa hilo, Neville Meena amesema
kuwa kitendo hicho si cha kukaliwa kimya kutokana na kukwaza utendaji wa
kazi na kudhalilisha utu wa waandishi hao mbele ya jamii.
Meena
amesema kuwa waandishi na wafanyakazi wa kituo hicho walikuwa katika
ofisi hizo za CCM, wakirusha na kuandika habari za tukio la mapokezi ya
Dk. John Magufuli baada ya kukabidhiwa hati ya ushindi wa urais na Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika hafla iliyofanyika siku hiyo katika
ukumbi wa Diamond Jublee.
“Kuzomewa
kwa waandishi hao katika ofisi za CCM ni muendelezo wa kile
kilichoanzia Diamond Jubilee ambapo wafuasi wa Chama cha Mapinduzi CCM,
walionekana wakiwazomea wafanyakazi wa ITV na baadaye kumzonga
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk Reginald Mengi ambaye ni mmliki wa kituo
hicho,” amesema Meena.
Ametoa
onyo kwa kuwataka wafuasi hao waache vitendo hivyo, akisema kuwa
utafiti mdogo waliofanywa na Jukwaa hilo kuhusu vitendo hivyo vinatokana
na wafuasi hao kuchukizwa na jinsi kituo hicho kilivyoripoti, matukio
ya kampeni na kuwapa fulsa wagombea wa vyama vingine vya siasa.
Amesema
kuwa kituo hicho ni miongoni mwa vyombo vya habari vilivyofanya kazi
zake kwa weredi wakati wa kampeni za wagombea wa vyama vyote nchi nzima
ambapo Dk. Magufuli na Mgombea Mwenza, Samia Suluhu walikuwa na wandishi
wa kituo hicho miongoni mwao ni Emmanuel Buhohera na Halfan Liundi
ambapo umma wa watanzania ulipata kufahamu kinachoendelea katika
mikutano yao ya kampeni.
Meena
ameongeza kuwa hilo sio tukio la kwanza kufanywa na chama hicho kwani
wakati wa kampeni za mgombea urais kilimfukuza katika msafara wa Dk.
Magufuli mkoani Mbeya, mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Peter Elias kwa
madai ya kutofurahishwa na habari aliyoandika kuhusu mgombea wao.
Amesema
kuwa matuko hayo siyo ya kiungwana na hayatakubalika katika jamii ya
watu wastaarabu. Ikiwa waandishi wa habari au vyombo vya habari
vinafanya makosa zipo njia za kisheria za kushughulikia makosa hayo
pamoja na kufanya mazungumzo kupitia taasisi za waandishi wa habari.
“Tunachukua
fulsa hii kuvitaka vyama vya siasa kama taasisi viongozi, wanachama na
wapenzi wake kuacha mara moja vitendo vya kuwashambulia waandishi wa
habari kwa sababu zozote zile. Tusingependa ifike hatua kutangaza kwamba
matukio ya chama fulani ni hatari kwa waandishi wa habari,” amesema Meena.
Kadhalika
tunachukua fursa hii kuvitaka vyama vya siasa na watu binafsi
wanaoandaa mikutano inayowahusisha waandishi wa habari kuhakikisha kuwa
waandishi wanakuwa salama wanapo hudhuria kwenye mikutano yao na
kuchukua hatua ya kukemea.
“Tunasikitika kwa ukimya wa chama hicho ulionyesha kufurahishwa kwa tukio hilo kutokana na kutotoa kauli yoyote,” amesema Meena.
Post a Comment