Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazee wastaafu, Wakulima na Wafanyakazi Zanzibar Mzee Ali Hassan Khamis akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hali ya nchi ilivyo sasa na kuwataka wananchi kusikiliza maelekezo yatakayotolewa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Picha na Makame/Maelezo Zanzibar.
RAMADHANI
ALI /MAELEZO ZANZIBAR
Jumuia ya
Wazee wastaafu, Wakulima na Wafanyakazi
Zanzibar imewashauri wananchi kuwa watulivu wakati huu na kusikiliza
maelekezo yatakayotolewa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) baada ya Menyekiti wa Tume hiyo kufuta uchaguzi Mkuu
uliofanyika tarehe 25.10.2015.
Akitoa tamko
juu ya hali halisi iliyojitokeza katika uchaguzi huo mbele ya waandishi wa
Habari, katika Ukumbi wa Redio Swahiba Migombani, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo
Mzee Ali Hassan Khamis alikubali kuwa uchaguzi umevurugika na lililobaki kwa sasa ni kusikiliza miongozo
ya ZEC ili kusawazisha kasoro iliyotokea.Mzee Ali
Hassan alisema Tume ya Uchaguzi ndio ya
kulaumiwa katika kuharibika kwa uchaguzi wa Zanzibar licha ya juhudi kubwa
iliyofanya ya kusimamia uchaguzi huo katika hatua za awali.
Alishauri kumalizwa tatizo lililopo na wananchi wenye wa Zanzibar
bila ya kushirikisha Jumuiya za Kimataifa kwani baadhi ya wakati maamuzi yao yanakuwa katika ushabiki wa
kisiasa.
Amesema Jumuiya
ya Wazee wastaafu, wakulima na
wafanyakzai inaunga mkono kurejewa kwa uchaguzi wa Zanzibar na hatua hiyo sio jambo kigeni kwa Zanzibar
kwa vile imewahi kutokea katika miaka ya siti.Mzee Ali
Hassan aliwapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kushiriki vizuri katika uchaguzi
huo kuanzia hatua ya kampeni na kupiga kura katika misingi ya amani na utulivu.
Aidha alimpongeza
Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa ushindi aliopata na
kuwataka wananchi wote kumuunga mkono katika juhudi za kuleta maendeleo kwa
wananchi wote.Aliwataka
viongozi wa vyama vya siasa na wananchi kwa kujumla kusahau tofauti zilizojitokeza wakati wa kampeni na wakati
wa kupiga kura na kuelekeza mawazo yao
katika kujenga Tanzania mpya.
Post a Comment