Katibu
Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole
Gabriel(wa kwanza kushoto) akiangalia mitambo ya kurushia matangazo ya
Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) wakati alipofanya ziara ya kikazi
katika minara ya shirika hilo leo hii Kisarawe.Profesa Elisante
amefanya ziara katika Taasisi tatu zilizo chini ya Wizara hiyo ambazo ni
Baraza la Sanaa Tanzabia (BASATA),Tanzania Standard Newspapers(TSN) na
Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) lengo likiwa ni kufahamiana na
wafanyakazi,kuwahimiza kufanya kazi kwa bidii na kujua changamoto
zinazowakabili ikiwa ni kutimiza kauli mbiu ya HAPA KAZI TU ya awamu ya
Tano.Anaefuatia ni mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bw.Clement Mshana.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole
Gabriel akiangalia tofauti ya santuri ya zamani na flashi ya kisasa
zinavyozidiana ukubwa kwa umbo alipotembelea maktaba mojawapo katika
ofisi za shirika la utangazaji Tanzania (TBC) alipofanya ziara kuongea
na menejimenti ya shirika ilo leo jijini Dar es Salaam.Santuri
zilitumika kipinda shirika hilo likiitwa Radio Tanzania Dar es Salaam
(RTD).
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole
Gabriel (waliosimama watatu kulia) akiwa katika mojawapo ya studio za
kurushia matangazo ya shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wwakati
alipotembelea shirika ilo leo kuongea na menejimenti yake pamoja na
kuona utendaji wake.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole
Gabriel (aliyekaa mwenye miwani) akipata maelekezo jinsi gazeti
linavyotengenezwa kutoka kwa mtumishi wa Standard News Papers(TSN) leo
jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kikazi na kuangalia utendaji wa
kazi.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole
Gabriel(wa pili kulia) akiangalia moja ya kazi za vijana wanojifunza
kutengeneza batiki na kuweka chapa alipotembelea ofisi za Baraza la
Sanaa Tanzania(BASATA) leo hii jijini Dar es Salaam.
Post a Comment