Marehemu, Rashid Saleh
Marehemu, Rashid Saleh
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye ni mlezi wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADU), akizungumza na Mkurugenzi
Mtendaji wa Global Pubrishers LTD, Eric Shigongo (katikati), na wadau
wengine kuhusu taratibu za mazishi za katibu huyo.
Mjumbe wa Chama
cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Stanley Kilave (kulia),
akizungumza na Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, Clement Masanja
(kushoto), pamoja na Mkurugenzi
Mtendaji wa Global Pubrishers LTD, Eric Shigongo (katikati), wakati wa
taratibu za mazishi zikifanyika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es
Salaam leo.
Msemaji
wa familia ya marehemu, Jonas Marinyizu (katikati), akitoa shukurani
kwa DC Makonda na wadau wengine kwa kuwezesha msiba huo pamoja na
utaratibu wa mazishi utakavyo kuwa.
Mwenyekiti wa Chama hicho, Shaban Mdem akizungumza katika mkutano na wanahabari
Mwenyekiti wa Chama hicho, Shaban Mdem akizungumza katika mkutano na wanahabari
Ndugu
na jamaa wa marehu wakiwa katika chumba za kuhifadhi maiti Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili wakisubiri kufanyika taratibu cha uchunguzi wa mwili
huo kabla ya kusafirishwa kwenda jijini Mwanza kwa mazishi.
Ndugu,
jamaa na marafiki wa marehemu wakiwa katika chumba za kuhifadhi maiti
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakisubiri kufanyika taratibu cha
uchunguzi wa mwili huo kabla ya kusafirishwa kwenda jijini Mwanza kwa
mazishi.
Na Dotto Mwaibale
MWILI
wa Katibu Mkuu na Msemaji wa Chama Cha Wafanyakazi Madereva Tanzania
(TADWU), Rashid Saleh umesafirishwa jana kwenda kijijini kwao Kayenze
wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza kwa maziko.
Saleh
alifariki jana Novemba 20 Majira ya saa 8 mchana katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH), wakati akipata matibabu ya maradhi ya figo ili
kuokoa maisha yake baada ya kile kinachodaiwa kushindwa kufanya kazi
ipasavyo.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ambaye pia ni
mlezi wa chama hicho, Paul Makonda alisema kuwa wamepata pigo kutokana
na umuhimu na umahiri ambao alikuwa nao marehemu hasa katika kutetea
haki za madereva wenzake sanjari na kuibua mambo mbalimbali ambayo
yatabaki kuwa historia na kumbukumbu kwao.
"Saleh
alifariki jana (Novemba 20) baada ya kusikia anaumwa ambapo hali yake
haikuwa nzuri na madaktari walishauri nimlete Muhimbili kwa matibabu
zaidi ambapo nilimfikisha lakini baada ya muda mfupi wakati madaktari
wanahangaika kumtibu na kuokoa maisha yake alifariki,"alisema.
Alisema
marehemu amekiacha chama sehemu ya mafanikio makubwa zaidi ya
mabadiliko na mikataba ya haki za madereva nchi nzima huku akibainisha
mazingira ya kifo na kutaka uchunguzi zaidi ili kujiridhisha na kifo
chake uliofanywa chini ya uangalizi wa polisi.
"Hatukuona
kama kuna haja ya kumuhifadhi mwili wa ndugu yetu hadi hapo tutakapojua
nini chanzo cha kifo chake kwani majibu ndiyo yatatupa picha ya ugonjwa
kwani tumehangaika tangu alipokuwa hospitali ya Kairuki ambapo
tulipofika hapa ikabainika kuwa figo zake zote mbili hazifanyi
kazi,"alisema.
Aliongeza
kuwa marehemu alipelekwa hospitalini hapo kwa kitengo maalum huku
akibainisha endapo figo zinashindwa kufanya kazi mzunguko mzima wa damu
mwilini nao husimama ambapo madaktari walishirikiana lakini hawakuweza
kuokoa maisha yake.
Mwenyekiti
wa Chama hicho, Shaban Mdem alisema kuwa msiba huo umewasikitisha sana
kutokana na mazingira ya kifo chake huku akiitaka mamlaka husika
kulisimamia suala hilo la kupatika kwa majibu sahihi juu ya kifo chake.
"Tunataka
uchunguzi ufanyike na majibu yatoke yakiwa sahihi na yanayoridhisha juu
ya kifo chake kwani amekufa na madai ambayo yapo ndani yao, hivyo
serikali itambue kifo cha Saleh ni katika harakati za kudai haki ambayo
tuliyawasilisha mbele ya aliyekuwa waziri mkuu Mizengo Pinda,"alisema.
Alisema
Saleh ni kiongozi wa taifa zima hivyo alimtaka rais Magufuli kuingilia
kati suala hilo kwani kutokana na hali hiyo watamaliza wafanyakazi wote
kwa kuwauwa katika mazingira kama hayo sambamba na kutenga siku rasmi
kwa ajili ya maombezo ya msemaji huyo.
Mazingira ya Kifo
Akizungumzia
mazingira ya kifo Msemaji wa Familia ya Marehemu Jonas Ernest alisema
kuwa Novemba 9 mwaka huu marehemu alipokea simu kutoka kwa rafiki yake
ma kumtaka waende kwenye kikao, ambapo baada ya hapo mwenzake alidai
kuwa na njaa.
Alidai
baada ya hapo walikwenda kuagiza chakula ambapo mwenzake hakula na
kumuacha marehemu akiwa anakula huku mwenzake akiwa amemuaga kwenda
msalani."Baada ya kurudi msalani alimkuta marehemu akilalamika tumbo
linamuuma na hivyo kuondoka eneo hilo pasi na huyo rafiki kula
chochote,"alisema.
Alidai
kuwa baada ya kuhisi maumivu makali ya tumbo alianza kuharisha na
kutapika na alikimbizwa hospitali lakini uchunguzi ulibaini hakuwa na
tatizo na kurudishwa nyumbani ambapo siku inayofuata alirudi hospitali
na kuambiwa kuwa ana malaria 4.
"Alianza
kutumia dawa za malaria na baadaye kujiskia vibaya na kumrudisha tena
hospitali ya Kairuki laikini madaktari walidai kuwa anatatizo ndani ya
mwili ambalo ni figo kushindwa kufanya kazi vizuri,"alidai na kuongeza
kuwa hadi marehemu anafariki alikaririwa akidai kuwa"Nyama
inanitenganisha na mwanangu lakini"na kumtaja mmoja wa wafanyakazi
wenzake huku akidai kumuona mtoto wake.
Harakati za kudai haki ya madereva
Saleh
alizaliwa mwaka 1966 Mwanza, ambapo hadi anafariki alikuwa katika
harakati za kudai na kutetea haki za madereva ambapo Oktoba 2, mwaka huu
alikaririwa akisema wamechoshwa na uozo unaoendelea kufanywa na Mamlaka
ya Usafirishaji Majini na Nchi Kavu (Sumatra) na Wizara ya Kazi na
Ajira kuhusu kufumbia macho kero zinazoitatiza sekta ya usafirishaji
hasa kwa madereva wa mabasi ya abiria na magari ya mizigo.
Post a Comment