Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Kobe 201 wakamatwa uwanja wa ndege wakisafirishwa nje ya nchi na Mabegi

Watuhumiwa hao wa usafirishaji wa wanyamapori wametajwa kuwa ni David Mungi mkazi wa
Muheza Mkoani Tanga na Mohammed Suleiman (43) mkazi wa Zanzibar ambao katika
tukio hilo walishafanikiwa kupita kwenye mitambo ya ukaguzi lakini mbwa maalum
(sniffer dogs) wakasaidia kugundua uhalifu huo. Kwa pamoja watuhumiwa hao
walikamatwa na tiketi za kusafiria kuelekea nchini Malaysia. Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Adelhelm Meru akikagua mabegi matano yenye Kobe 201 yaliyokamatwa usiku wa kuamkia leo na askari wanyamapori kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na
usalama katika uwanja wa Kimataifa wa J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam.  Kobe wapatao 201 waliokamatwa na askari wanyamapori kwa ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutumia mbwa maalum (sniffer dogs)Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Dorina Makaya kulia na Mmoja wa Askari wanyamapori wakiangalia kobe 103 waliotelekezwa eneo la Tabata hivi karibuni baada wahalifu waliohusika kuhofia kukamatwa na vyombo vya dola. (Picha na Hamza Temba - Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii)
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top