Waziri
mkuu mstaafu Mh.Edward Lowassa amewatembelea na kuwapa pole wahanga
wanne waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga
baada ya kunusurika kufa katika machimbo ya Nyangalata wilayani humo.
Mh.
Lowassa amefika hospitalini hapo akitokea jijini Mwanza na kupokelewa
na uongozi wa hospitali hiyo ambao walimuongoza hadi kwenye vitanda
walipokuwa wamelazwa wahanga hao wa machimbo ya Nyangalata.
Post a Comment