Aliyekuwa mgombea wa urais kupitia
Chadema na Ukawa, Edward Lowassa amesema ataendelea Chadema na Ukawa, Edward Lowassa amesema ataendelea
kushiriki kikamilifu katika siasa na kubainisha kuwa
utaendeleza mapambano ya mabadiliko kwa kudai Katiba Mpya.
Lowassa aliwaambia wanahabari leo kuwa kasi ya ufanyaji wa
siasa itaongezeka kuliko ilivyokuwa awali na kwamba kwa sasa
anaweza akawa “amepoteza pambano lakini siyo vita.”
Kauli hiyo ya Lowassa inabadilisha msimamo wake wa awali aliokuwa wameutangaza kupitia
mahojiano na Shirila la Habari la Uingereza (BBC) kuwa iwapo angeshindwa kinyang’anyiro hicho
cha urais angeenda kuchunga ng’ombe kijijini kwake Monduli mkoani Arusha.
Mwanasiasa huyo, ambaye pia ni waziri mkuu wa zamani, alisema Ukawa itaendelea kudai Katiba
Mpya ya wananchi itakayohakikisha kuwa Tanzania inakuwa na tume huru ya uchaguzi na serikali
inayowajibika kwa umma.
“Ni wazi kuwa uchaguzi mwingine katika mazingira ya sasa na chini ya katiba ya sasa hauwezi
kuzaa matunda tofauti.
Bila katiba mpya ya wananchi, Tanzania haitakuwa na demokrasia na
itaendelea kuwa nchi inayotawaliwa kwa mizengwe na udikteta wa CCM,” alisema Lowassa.
TAARIFA KAMILI HII HAPA ...
Ndugu Watanzania wenzangu
Kama
nilivyo waambia Viongozi Wakuu wa UKAWA walikaa juzi kutafakari hali ya
kisiasa nchini na hususan Zanzibar na matukio yaliyoandamana na
Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktober mwaka huu.
Wakuu
wa UKAWA kwa kauli moja walikariri tamko lao la kumuunga mkono kwa
dhati, Mh. Maalim Seif Sharif Hamad kwa ushindi wake dhahiri na kuitaka
Tume ya Uchaguzi Zanzibar imtangaza kuwa Rais wa Zanzibar mara moja.
Viongozi
wa UKAWA walilaani vikali uamuzi wa ZEC kufuta uchaguzi halali na
wakaonya kuwa mbinu mpya za kutaka uchaguzi urudiwe hazikubaliki na
zitahatarisha amani na utilivu Zanzibar. Viongozi wa UKAWA walimpongeza
Maalim Seif na viongozi wote wa CUF Zanzibar kwa busara na ustahimili
wao mkubwa na jitihada zao zinazoendelea kulinda amani na utulivu nchini
humo.
Kinyume
na Tanzania bara, uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa wa wazi na wa amani.
Vyama vyote vya siasa na hata wawakilishi wa Kimataifa walikiri hivyo
mpaka pale ilipobainika kuwa CCM inashindwa. Wakuu wa UKAWA walikataa
dhana kuwa uchaguzi ule ule unaodaiwa kufutwa kwa kuwa ulikuwa na
mizengwe, ulizaa matokeo halali wa Wawakilishi wa Bunge la Jamuhuri ya
Muungano na ya Urais wa Tanzania lakini batili kwa wajumbe la Baraza la
Wawakilishi na Rais wa Zanzibar. Dhana hii haina mantiki yoyote bali ni
ubabe wa kisiasa tu.
Haiwezekani
chungu kimoja kikapika halali na haramu kwa pamoja. Kwa kigezo cha ZEC
kuwa uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa batili basi matokeo yake yote ikiwa ni
pamoja na yale ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano pia ni batili. Hii ina
maana kuwa hata ushindi unao-daiwa na Bwana Magufuli, mbali ya kuwa ni
matokeo haramu ya wizi kwa kura za Tanzania bara, pia ni batili kisheria
kwani hana ridhaa ya watu wa pande zote mbili za Muungano.
Aidha
kwa kauli moja Wakuu wa UKAWA walikubaliana kuwa hali si shwari nchini
licha ya ukimya wa Wananchi. Wananchi wanaelewa fika kuwa CCM na
Serikali yake wamepora ushindi wao na sasa inaendelea kushinikiza kwa
vitisho vya majeshi yenye silaha yanayoranda mitaani ili matokeo ya wizi
huo wa waziwazi yakubalike. CCM na serikali yake wanajua kuwa
haikubaliki na hata ifanye vipi haiwezi kushinikiza nafsi za Watanzania.
Kama
CCM inadai kuwa imeshinda kwa nini ihitaji majeshi, magari ya washa
washa na silaha za vita ili wakubalike? CCM ilitayarisha mkakati wa
kuhujumu uchaguzi na ndiyo maana ikanunua magari, na vifaa vya vita kwa
mabilioni ya fedha ili kuutisha Umma wakati wananchi wanakufa kwa kukosa
dawa na huduma hospitalini. Kama CCM inadai imeshinda kwa nini wana
hofu kubwa mpaka kuhujumu uhuru wa vyombo yva habari, kupiga marufuku
mikutano ya kisiasa na kutunyima viongozi wa UKAWA hata fursa ya
kuwashukuru Wananchi kwa kutuunga mkono katika safari yetu ya kuleta
mabadiliko?
Hii ni aibu kwa taifa letu.
Tuna
ushahidi wa kutosha kuonyesha jinsi matokeoa ya Uchaguzi wa Rais wa
Jamuhuri ya Muungano yalivyochakachuliwa na kiasi cha kura zilizoibiwa.
Wakati muafaka tutaweka bayana ushahidi huo ili Watanzania wajue kwa
nini UKAWA inasema kwa dhati kuwa haitambui matokeo yaliyotangazwa na
Tume ya Uchaguzi na kwa nini haitashirikiana na serikali ya sasa ambayo
ni batili kisheria. Kama sheria ingeturuhusu tungekuwa mahakamani
kupinga uamuzi wa Tume ya Uchaguzi. Uamuzi huo umetekelezwa tu kwa
sababu ya fitna ya sheria mbovu zilizotungwa kuhakikisha kuwa CCM
inabaki madarakani milele. Hii lazma tuendelee kuikataa na kuipinga kwa
nguvu zetu zote.
UKAWA
itaendelea kuwataka Watanzania wakatae matokeo batili ya Uchaguzi Mkuu
wa Tanzania Bara na waendelee kuwa watulivu. UKWAWA itaendeleza harakati
za kisiasa katika nyanja mbalimbali ili kutekeleza azma ya kuleta
mabadiliko ya kweli nchini.
Aidha
UKAWA itaendelea kudai Katiba ya Wananchi itakayohakikisha kuwa
Tanzania inakuwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Serikali inayowajibika kwa
Umma. Ni wazi kuwa uchaguzi mwingine katika mazingira ya sasa na chini
ya Katiba ya sasa hauwezi kuzaa matunda tofauti. Bila Katiba mpya ya
Wananchi, Tanzania haitakuwa na demokrasia na itaendelea kuwa nchi
inayotawaliwa kwa mizengwe na udikteta wa CCM.
Asanteni sana.
Post a Comment