Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mahakama yaamuru Mzee aliyefanyiwa unyama Arusha arudishiwe nyumba yake

 
 
Mahakama ya ardhi na nyumba mkoa wa Arusha imeamuru mzee wa miaka themanini Juma Isangu aliyeondoshwa kwa nguvu katika nyumba yake arudi kwenye nyumba yake na arudishiwe vyombo vyake wakati ikisubiriwa kuanza kusikilizwa kwa shitaka la msingi huku Bi Jane Fosbroke na wakala wa mahaka majembe Auction Malt wakitakiwa kulipa ghalama za usumbufu kwa mzee Juma Isangu.

Akitoa amri hiyo mwenyekiti wa mahakama ya ardhi na nyumba mkoa wa Arusha Cyriacus Kamugisha amesema kutokana naombi liliowakilishwa na upande wa mashitaka mahakama imeyapitia kujirishisha na kufanya uamuzi huo kwa kuzingatia misingi ya kisheria.
 
Wakizungumza baada ya kutoka kwa amri hiyo mawakili wa wanao mtetea mzee Juma Isango Willifredy Milambo na Loam Ojale wamesema wamezidhika na uamuzi wa mahakama kwakuwa awali mteja wao hakutendewa haki kwa kuondoshwa kwa nguvu katika nyumba yake  huku akiwa na nyalaka zilizo halali huku Bi Janeth akieleza kutoridhishwa na uamuzi wa mahakama.
 
Kwa upande wao watetezi wa haki za wazee wamesema ikiwa mahakama zitafanyakazi kwa uadilifu na kuharakisha maauzi kama ilivyo fanya kwa mzee huyo zitarudisha imani kwa wananchi huku wakiipongeza mahakama hiyo kutenda haki kwa mzee Isangu na majira wa mzee huyo ambayo wamehifadhi familia yake baada ya kunyanganywa nyumba wametoa shukurani kwa uamuzi uliyo tolewa na mahakama ikiwa ni pamoja na kumpatia wakala wa mahakama atakaye rudisha vyombo vya mzee Isangu
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top