Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAKAMU WA RAIS, MAMA SAMIA SULUHU AKABIDHIWA RASMI OFISI, AKARIBISHWA RASMI NA WAFANYAKAZI WA OFISI YAKE


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akipokea nyaraka za Ofisi kutoka kwa Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,leo. Picha zote na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akisaini Kitabu cha wageni wakati alipoingia Ofisini kwake kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo Nov 9, 2015  Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia kwake), Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula na Naibu Katibu Mkuu wake, ....baada ya makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi Binafsi ya Makamu wa Rais, baada ya bakabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi Binafsi ya Makamu wa Rais, baada ya bakabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo
 Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi Binafsi ya Makamu wa Rais, wakati akiondoka baada ya makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo.
 Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakiwa wamejipanga mstari wakisubiri kumpokea Bosi wao Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akiwasili leo kwa mara ya kwanza baada ya makabidhiano rasmi ya Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Bilal.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi ya Maua kama ishara ya makaribisho, kutoka kwa mfanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Martha Mashuki, wakati alipowasili kwa mara ya kwanza kwenye Ofisi yake na kupokelewa na wafanyakazi wake leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ua Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan,akisalimiana na Katibu Mkuu wa Ofisi yake, Sazi Salula,wakati alipowasili kwenye Ofisi yake kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa ofisi rasmi leo, Nov 9,2015. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Eng. Angelina Madete.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi yake wakati alipowasili kwenye Ofisi yake kwa mara ya kwanza leo baada ya kukabidhiwa rasmi Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Bilal. Wafanyakazi hao walijipanga kumpokea huku wakiimba, kupiga makofi na vigeregre wakati akiwasili.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi yake wakati alipowasili kwenye Ofisi yake kwa mara ya kwanza leo baada ya kukabidhiwa rasmi Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Bilal. Wafanyakazi hao walijipanga kumpokea huku wakiimba, kupiga makofi na vigeregre wakati akiwasili.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati alipowasili kwenye Ofisi hiyo leo Nov 9, 2015 baada ya makabidhiano. Akizungumza na wafanyakazi hao Mama Samia, aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa mashirikiano na kwa bidii ili kutimiza Kaulimbiu ya Mhe.Rais ya 'HAPA KAZI TU'.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza nao leo alipowasili Ofisini kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa Ofisi rasmi. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara zilizo chini ya Ofisi ya makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) alipowasili ofisi kwake kwa mara ya kwanza leo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi yake baada ya kuzungumza nao alipowasili ofisi kwake kwa mara ya kwanza leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wanamama wa Ofisi yake baada ya kuzungumza nao alipowasili ofisi kwake kwa mara ya kwanza leo Nov 9, 2015 kwa makabidhiano ya Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top