THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SALAMU ZA PONGEZI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli amepokea salamu za pongezi kutoka kwa Malkia Elizabeth II wa
Uingereza kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Katika salamu hizo Malkia wa Uingereza amemueleza Mhe. Rais Dkt.
Magufuli kuwa “Natumaini kuwa mahusiano baina ya nchi hizi mbili ambazo
ni wanachama wa Jumuiya ya Madola yataendelea wakati wa utawala wako,
nakutakia kheri pamoja na wananchi wa Tanzania” amesema malkia katika
salamu zake.
Salamu pia zimetoka kwa Mfalme Akihito wa Japan ambaye amemueleza
Mhe. Rais Dkt. Magufuli “Nakutumia salamu za dhati, mafanikio na
furaha kwako Mheshimiwa Rais na watu wa nchi yako” Amesema.
Salamu zingine kwa Mhe. Rais Dkt. Magufuli zimetoka kwa Rais wa
Jamhuri ya kidemokrasia ya Kiarabu ya Saharawi, Mhe. Mohamed Abdelaziz
ambaye amemtakia kheri Mhe. Rais Dkt. Magufuli na kumueleza kuwa “Nina
imani kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea vyema chini ya
uongozi wako kuelekea katika kupata maendeleo na mafanikio zaidi”.
Amesema;
na pia amekipongeza Chama Cha Mapinduzi na Watanzania kwa uchaguzi wa
kidemokrasia ulioendeshwa katika mazingira ya kistaarabu chini ya
usimamizi wa waangalizi kutoka kwenye kanda, bara na kimataifa na hivyo
kuliletea sifa bara la Afrika.
Mhe. Rais Dkt. Magufuli pia amepokea salamu kutoka kwa Rais wa
Namibia Mhe. Hage Geingob na kumueleza Mhe. Rais Dkt. Magufuli kuwa
salamu zake na zile za wananchi wa Namibia ni za dhati kwa Serikali na
Watanzania kwa ujumla kwa ushindi wa kiti cha Urais.
“Pia napenda kutoa pongezi kwa Chama Cha Mapinduzi kwa ushindi
uliopatikana katika uchaguzi wa Oktoba 25, 2015”. Amesema na kuongeza
kuwa “Kwa hakika Watanzania wamezungumza na kukipa tena CCM Mamlaka ya
kuipeleka mbele Tanzania kuelekea kwenye mafanikio zaidi”. Ameongeza.
Salamu zingine ni kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye
amesema Tanzania kwa mara nyingine tena imedhihirisha kuwa ni nguzo ya
demokrasia barani Afrika.
Naye Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Joachim Gauck
amemtakia Mhe. Rais Dkt. Magufuli na Watanzania kwa ujumla mafanikio
katika kuendeleza Taifa kwa ujumla.
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
16 Novemba, 2015.
Post a Comment