Mashabiki hao wamepokea tofauti taarifa ya kukatwa kwa jina la Irene Uwoya katika katika vitu maalumu, wapo ambao wameonyesha kuguswa na kuumia Irene Uwoya kushindwa ingawa lipo kundi lingine ambalo linaonyesha kufurahia taarifa ya kushindwa kwa msanii huyo ambaye alikuwa moja ya watu ambao walikuwa wakifanya kampeni za uchaguzi kupitia Kundi la Kibajaji.
Yafuatayo ni maoni mbalimbali ya mashabiki wa ukurasa wa facebook wa EATV kwa Irene Uwoya.
Neema Mgwale: “Hahahaa afadhali kashindwa maana alivyokuwa anashoboka na kuwatukana wasanii wa UKAWA na nilimuona anawaambia wasanii wa UKAWA eti wamemsaliti Jakaya Kikwete kwani alikuwa anawaita Ikulu kila siku yaani hapo ndo nilimwona hafai sababu anathamini kula na rais Ikulu kuliko maisha magumu ya watanzania aendage tuu siasa haimfai”.
Kwa upande wa shabiki mwingine alikuwa na haya ya kusema. “Amshukuru Mungu wake na aamini kuwa kila likuepukalo lina kheri na yeye, kwa sababu CCM inahitaji kubadilisha muelekeo wa bendera yake na kwa sababu hiyo watu wa mzaha mzaha mwaka huu hawana nafasi miaka hii 5 ndio Interview ya CCM kuangalia kama tuwape tena au tusiwape kabisaa na ukumbuke kwenye Interview hatumwi mtoto” ameandika Enock Kayagambe Yahaya.
Post a Comment