POLE!
Staa mwenye mvuto ndani ya Bongo Muvi, Kajala Masanja hivi karibuni
alipata pigo zito baada ya kufiwa na bibi yake (mzaa mama) aliyekuwa
akiuugua kwa muda mrefu huko mkoani Songea.
Akizungumza
na Ijumaa Wikienda akiwa msibani, Kajala alisema amempoteza mtu muhimu
katika maisha yake kwani bibi yake huyo alikuwa akimpenda, kumlea na
kumshauri mambo muhimu kwenye maisha.
Kajala
alifunguka kuwa alipopata taarifa za msiba wa bibi yake alihisi
kuchangayikiwa na maumivu yaliyosababisha mapigo ya moyo kupanda
(presha).
“Siwezi kueleza ni jinsi gani nilikuwa nikimpenda bibi yangu, alikuwa ni msaada mkubwa sana kwangu.
Kila nilipotatizika na jambo lolote sikusita kumfuata na kumshirikisha, kiukweli ni pigo kubwa sana kwangu,” alisema Kajala.
Post a Comment