Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli
akikagua gwaride maalum la Jeshi la Ulinzi lenye Umbo la Alfa, ikiwa ni
ishara ya kuanza kwa Serikali mpya ya awamu ya tano, katika Sherehe za
kuapishwa kwake, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es
salaam leo. Sherehe hizo zimehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa ndani
na nje ya nchi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akila
kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mh. Mohamed Chande Othman, katika
Sherehe za kuapishwa kwake, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini
Dar es salaam leo.Kushoto ni Rais aliemaliza muda wake, Mh. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Makamu wake, Mh. Dkt. Mohamed Gharib
Bilal. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
Rais
aliemaliza muda wake, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davies Mwamunyange, wakati
akiwaaga wananchi mara tu alipowasili kwenye Uwanja wa Taifa, katika
Sherehe za kuapishwa Rais Mpya wa awamu ya tano, Mh. Dkt. John Pombe
Magufuli, zilizofanyika leo jijini Dar es salaam.
Rais
aliemaliza muda wake, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea salamu ya
heshima ya kijeshi kabla ya kukabidhi madaraka kwa Rais Mpya wa awamu
ya tano, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais
Mpya wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John
Pombe Magufuli akionyesha Mkuki na Ngao aliokabidhiwa na Wazee wa
kimila ikiwa ni ishara ya Uongozi wa Kitaifa, katika Sherehe za
kuapishwa kwake, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es
salaam leo.
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiapishwa kuwa Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uwanja wa Uhuru leo.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwa amekaa na viongozi mbalimbali
katika jukwaa kuu mara baada ya kuapishwa leo hii kwenye uwanja wa
Uhuru jijini Dar es salaam.
Kadinali Policarp Pengo na Askofu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya
Mashariki na Pwani Dk. Alex Malasusa wakielekea katika eneo la
kuapishia.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande na Spika wa Bunge mama Anne Makinda wakielekea katika aneo la kuapishia.
Viongozi mbalimbali serikali na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwa katika sherehe hizo kwenye uwanja wa Uhuru.
Chanzo: Michuzi Jiachie blog
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uwanja wa Uhuru leo.
Post a Comment