Mawaziri
sita wajiuzulu kutoka katika Chama cha upinzani CUF, mawaziri hao
wamechukua hatua hiyo kutokana na msuguano wa kisiasa visiwani humo.
Waziri
wa sheria na katiba Abubakar Khamis Bakary alitoa kauli hiyo wakati
akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya maazimio yaliyofikiwa na
baraza la chama la Halmashauri kuu ya Taifa.
Mawaziri
wengine waliojiuzulu ni Fatma Abdulhabibu Fereji,Waziri wa Nchi ofisi
ya Makamu wa Rais wa kwanza, waziri wa Biashara, Viwanda na Makoso
Nassor Ahmed Mazrui, Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni
Haji, Waziri wa afya Rashidi Suleiman na Waziri wa Uvuvi na Mifugo
Abdillah Jihadi.
Na
wengine ni, Haji Mwandani Makame aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi na
Nyumba, Maji na Nishati, Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo Zahara Ali
Hamed na Naibu Waziri wa Kilimo Maliasili Mtumwa Kheir Mbarak.
Kwa
mujibu wa Abubakary kila Waziri na Manaibu wao wamekabidhi magari ya
serikali na vifaa vingine kwa mamlaka na kwa mujibu wa kifungu cha
sheria cha (28) ya katiba ya Zanzibar, umiliki wa ofisi kwa ajili ya
wote akiwemo na Rais Dr Ali Mohamed Shein na mawaziri kumalizika Novemba
2.
Post a Comment