WAKATI Rais
John Pombe Magufuli akitegemewa kutangaza Baraza la Mawaziri wakati
wowote kuanzia sasa, matumbo ya wabunge yamepata moto wakijiuliza kama
watawezana na kasi yake endapo watateuliwa kuwemo.
Magufuli,
ambaye Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alimuita Tingatinga, ameweka wazi
katika hotuba yake kwa Bunge kuwa hatamvumilia mtu mzembe na mvivu na
kwamba watakaobainika kujihusisha na rushwa au ufisadi,
watashughulikiwa.
Ingawa
wabunge karibu wote walikuwa wakimshangilia kwa nguvu wakati wa hotuba
yake hiyo, inadaiwa hamu ya kupata ulaji wa uwaziri inawafanya baadhi
yao kuingiwa na woga, kwani ufanyaji kazi wa mazoea ndiyo unaowatesa.
“Nakuambia
hapa wabunge, hasa wale wenye ndoto za kuteuliwa uwaziri wana wasiwasi
kama wataweza kweli kwenda na kasi ya huyu jamaa, maana anaonekana kuwa
siriaz sana na kazi. Hili liko wazi maana wengi walizoea kuona nafasi za
juu kiuongozi wanazitumia kwa masilahi yao,” kilisema chanzo chetu
katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Inadaiwa
wengi wa wanaotegemea kupata uwaziri wana hofu kwa sababu wanaamini
mzigo watakaopewa utakuwa mkubwa kuliko tabia na hulka zao.
Rais
Magufuli ameahidi kuteua Baraza dogo la Mawaziri litakalokuwa
limesheheni wachapakazi na katika kukabiliana na vitendo vya rushwa na
ufisadi, alisema kazi hiyo ataifanya kwa dhati.
Hata
hivyo, mbali na jina la Tingatinga hivi sasa mtaani amepewa jina jipya
la Mtumbua majipu licha ya kuwa kitendo hicho huleta maumivu.
Post a Comment