Mwenyekiti
wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP),Agustino Lyatonga
Mrema akizungumza leo na waandishi habari juu ya kufanyiwa rafu katika
jimbo la vunjo na kusababisha kushindwa kulitwa kwa mara nyingine
kushoto ni aliyekuwa Mgombea Urais wa TLP ,Maxmillian Lyimo , na Kulia
Katibu Mkuu wa TLP,Nancy Mricaria.
Mwenyekiti
wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Agustino Lyatonga
Mrema akionyesha moja ya kipeperushi kilichomsababisha kukosa jimbo hilo
kushoto ni aliyekuwa Mgombea Urais wa TLP, Maxmillian Lyimo , na Kulia
Katibu Mkuu wa TLP, Nancy Mricaria.
Mwenyekiti
wa Umoja Wanawake wa Vunjo,Venancia Nicholaus akizungumza na waandishi
juu ya wanawake wa vunjo walivyopata pigo kuungushwa kwa mgombea wao
Mrema kwa hujuma za Mbatia kulia ni Mgombea Ubunge Bunda Mjini,Dk.Lucas
Webiro leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi
wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Tanzania
Labour Party (TLP), Agustino Lyatonga Mrema leo jijini Dar es Salaaam.
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii
******
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MWENYEKITI
wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Agustino Lyatonga
Mrema amesema kuwa kushindwa kwake ubunge kulitokana na michezo mchafu
uliochezwa na mshindi wa ubunge wa jimbo hilo, Mwenyekiti wa Taifa wa
Chama cha NCCR-MAGEUZI, James Mbatia
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mrema amesema kuwa
mshindi wa jimbo hilo amekuwa akionywa na msimamizi wa uchaguzi
kutokana na matumizi ya vipeperushi ambavyo yeye alijipigia kura ya
ubunge katika jimbo la Vunjo.
Mrema
amesema matokeo ya yaliyompa ushindi Mbatia hakusaini kutokana na
kufanya hujuma nyingi ikiwa ni pamoja na kumsema mgombea mwenzake.
Aidha
amesema kuwa katika kipeperushi chake Mbatia sehemu ya bendera ya TLP
yenye alama ya jogoo ilionekana kifaranga baada ya kuwa na jogoo mkubwa
anayewika.
Mrema
katika kukutana na waandishi pia alimpongeza Rais Mteule wa CCM,
Dk.John Pombe Magufuli kwa kura za kishindo na kutaka kuwa yuko naye.
Amesema
kumpigia kampeni Mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli kulitokana na
kazi nzuri ya kupeleka barabara katika jimbo lake akiwa Waziri wa
Ujenzi.
Post a Comment