Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt. James
Mataragio akuzungumza mbele ya waandishi wa habari kuhusu ujio wa ndege
ya pili ya utafiti wa awali wa mafuta na gesi asilia katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mwishoni mwa wiki, ndege hiyo
inatarajia kuanza utafiti wiki hii katika kitalu cha Eyasi Wembere na
Mandawa.
Mkurugenzi
Mtendaji TPDC Dkt. James Mataragio akipatiwa maelekezo ya jinsi ndege
hiyo inavyofanya kazi (ndani ya ndege) kutoka kwa Meneja wa Mradi Brett
Robinson wa kampuni inayoendesha utafiti huo ya “CGG AVITION LTD”
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), utafiti huo
unagharamiwa na TPDC kutoka katika mfuko wa fedha za maendeleo.
Ndege
ya utafiti wa awali wa mafuta na gesi asilia inayotarajia kuanza
utafiti katika kitalu cha Eyasi Wembere na Mandawa ikiwa katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Mkoani Kilimanjaro mwishoni
mwa wiki.
Meneja
wa Mradi Brett Robinson wa kampuni inayoendesha utafiti huo ya “CGG
AVITION LTD” (kushoto) akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari
jinsi ndege hiyo itakavyofanya utafiti, Mkurugenzi Mtendaji TPDC Dkt.
James Mataragio (kulia).
Post a Comment