Baada ya mtandao wa Billboard kuachia orodha ya 10 greatest rappers of all time, maneno mengi yaliibuka juu ya ukweli ya orodha hiyo huku watu wengine kama Snoop Dogg walidai kutokuwepo kwa 2 Pac kwenye orodha hiyo ni kitendo kinachoishushia heshima muziki wa Hip Hop wa Marekani… hali hii Bongo Flevani ipoje!?
Msanii wa muziki wa HipHop, Tanzania kutoka kwenye kundi la WEUSI, Nikk wa Pilli ameamua na yeye kupost list ya MC’s wakali zaidi kwa Tanzania kupitia page yake ya Instagram! List hiyo imepewa jina Top Ten MC’ Of All Timez…TZ, ungependa kujua list hiyo imebeba majina ya watu gani?!
Kwenye list ya Top Ten MC Of All Timez Tz ya Nikk wa Pili watu kama Professor Jay, Sugu, Ngwea, Mwana FA na Fid Q hawakosekani…
lakini hawa ni watu 5 tu kwenye orodha ya Nikk wa Pili, wengine je?…
Unaweza kukutana na majina ya wakali wote hapa chini kwenye hii post
nilioweza kuinasa kupitia page yake ya Instagram @nikkwapili…
TOP TEN MC ‘ OF ALL TIME…. Tz (kwa mujibu wa Nikk wa Pili) ni…
- SUGU
- Professor Jay
- Ngwea.
- Joh Makini.
- Mwana FA.
- Fid Q.
- AY.
- Lord IZ.
- Jay Mo
- Nikk wa Pili.
Hiyo ndio list ya Nikk wa Pili mtu
wangu, ipoje? unakubaliana nayo? Kama kuna mtu amekosekana hapa,
unahisi ni nani? Ongea na mimi kwa kunipa comment yako hapa chini.
Post a Comment