Promoter
"DMK" wa Kampuni ya DMK GLOBAL PROMOTIONS ashinda Tuzo ya Best Promoter
USA katika zile tuzo za AFRICAN ENTERTAINMENT AWARDS USA 2015 ,Tuzo
hizo zilitolewa OCTOBER 31 New York ambapo Makampuni 6 yalikuwa
yakichuana kipengele hicho na DMK Global kuibuka kidedea,Pia katika
Awards hizo Wasanii kutoka Tanzania Diamond alichukua Tuzo ya Hottest
Male Single na Ommy Dimpoz tuzo ya People's Choice .
Kampuni hii inafanya Shuguli zake Marekani za kuandaa Events mbali
mbali za burudani kama CLUB EVENT,CONCERTS, CARNIVALS ikiwa ni pamoja
na kuleta wasanii Marekani kutoka Tanzania na Africa kwa ujumla,pia
inafanya matamasha ya Burudani na wasanii wa Marekani pia.Baada ya Tuzo
hizi Tulimpigia simu bwana DMK na kumpongeza kwa kuiwakilisha vyema
Tanzania na East Africa kwa ujumla ambapo aliwashukuru sana waliompigia
kura kote Duniani na kuongezea kuwa Tuzo hii ameipata yeye lakini
angependa ijulikanekuwa shughuli hizi huwa anazifanya kwa kusaidiana na
Partners wake kampuni za Safari Entertainment na J&P Ent ambazo
amesema kuwa bila wao kushurikiana nao asingekuwa hapo alipo.
Bwana DMK amesema tutegemee Mambo makubwa mengi kutoka kwake na Partners wake hivi Karibuni.
Post a Comment