Katika
salamu hizo Rais Magufuli amesema taifa limempoteza mtu shupavu,
mkweli, makini na aliyependa kupigania haki pale alipoamini kuwa
panastahili haki hiyo na alithibitisha kwa kupigania uanzishwaji wa
Chama Cha Madereva na kusimama kidete kutetea haki zao.
"Nawatakia
moyo wa uvumilivu familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki,
madereva na wengine wote ambao wameguswa na kifo cha Rashid Salehe na
wote tuungane kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ampumzishe mahali pema
peponi".
Marehemu Rashid Salehe enzi za uhai wake.
Dr
Magufuli anaungana na wote walioguswa na msiba huo katika kipindi hiki
kigumu na kwamba taifa litauenzi mchango mkubwa alioutoa marehemu Rashid
Salehe.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi Mawasiliano, IKULU
23 Novemba, 2015.
Post a Comment