Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Spika wa Bunge Job Ndugai awa mbogo .... awapa UKAWA onyo la mwisho

Spika wa Bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai ameelezwa kusikitishwa kitendo kilichofanywa na baadhi ya wabunge kuzomea.

Amesema kitendo hicho siyo cha kiungwana na hivyo kulazimika kuwaomba radhi viongozi kutoka zanzibar na kuahidi kitendo hicho hakitajirudia tena.

Amesema wabunge waliomchagua wanaweza kumfanya awe spika mwema na mzuri 

Awali wakati wa kuwakaribisha viongozi mbalimbali akiwemo rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh John Magufuli na rais wa Zanzibar mh Dkt Ally Muhamed Shen ndipo viongozi hao wakaanza kupika kelele.


Wakati wa kumkaribisha rais wa zanzibar baadhi ya wabunge waliendelea kupiga kelele na hivyo kumlazimu spika wa bunge kuwataka watoke nje nao wakafanya hivyo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top