Mkurugenzi
Mkuu wa Hifadhi za Taifa Bw. Allan Kijazi akikabidhi cheti cha kuhitimu
mafunzo ya uongozi kutoka mfumo wa kiraia kwenda jeshi-usu kwa Mhifadhi
Mussa Mandia katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Hifadhi za Taifa Bw. Allan Kijazi akikabidhi zawadi ya kuhitimu
mafunzo ya uongozi kutoka mfumo wa kiraia kwenda jeshi-usu kwa Mhifadhi
Prisca Lyimo katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii Bw.
Faustine Masalu akiongea wakati wa hafla ya ufungaji wa mafuzo ya kutoka
mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa wa jeshi-usu.
Meneja
Ulinzi wa Hifadhi za Taifa Bw. Emily Kisamo akitoa maelezo ya mafunzo
ya kubadili mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa wa jeshi-usu kwa mgeni
rasmi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Hifadhi za Taifa Bw. Allan Kijazi akiongea wakati wa hafla ya
ufungaji wa mafunzo kubadili mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa wa
jeshi-usu.
Mkurugenzi
Mkuu wa Hifadhi za Taifa Bw. Allan Kijazi akifungua mafunzo ya awamu ya
pili mafunzo kubadili mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa wa
jeshi-usu.
Wahifadhi waliohitimu mafunzo kubadili mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa wa jeshi-usu wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkurugenzi
wa Utumishi na Utawala wa TANAPA Bi. Witness Shoo akiwa na Wahifadhi wa
kike waliohitimu mafunzo ya kubadili mfumo wa utendaji kazi wa kiraia
kuwa wa jeshi-usu.
Mkurugenzi
Mkuu wa TANAPA Bw. Allan Kijazi akikagua gwaride maalum la wahitimu
huku akiongozwa na Kamanda wa Gwaride hilo Mhifadhi Kelvin Nkulila.
Gwaride la wahitimu wa mafunzo kubadili mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa wa jeshi-usu likitoa heshima mbele ya mgeni rasmi.
Mmojawapo wa wahitimu akilenga shabaha.
****
Shirika
la Hifadhi za Taifa limeanza rasmi kutumia mfumo wa jeshi usu kutoka
ule wa kiraia katika utendaji kazi wake ikiwa ni hatua mojawapo ya
kuongeza ufanisi katika shughuli za uhifadhi.
Jumla
ya wahifadhi 40 walihitimu mafunzo ya Awamu ya kwanza ya kubadili mfumo
wa utendaji kazi kutoka ule wa kiraia kwenda wa jeshi usu kwa kwa
viongozi maafisa wa ngazi ya kati “Transformation Leadership Course for
Middle Cadre Wardens” yaliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi
hivi karibuni.
Mfumo
wa utendaji kazi kwa kijeshi-usu utalisadia shirika kuimarisha nidhamu
ili kuboresha utendaji kazi hasa katika nyakati hizi ambapo changamoto
kuu ya ujangili unaotumia silaha za aina mbalimbali za moto hasa za
kivita inazidi kushika kasi.
Post a Comment