TAARIFA YA HITILAFU ZA UMEME ZILIZOSABABISHWA NA MVUA ZILIZONYESHA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM TAREHE 5 NOVEMBA 2015
Pamoja
na ukweli kwamba Shirika lilikuwa limewaweka tayari mafundi katika
mikoa yote kukabiliana na tatizo lo lote la umeme, hali hiyo ya mvua
ilifanya umeme kukatika katika maeneo mengi.
Baadhi
ya maeneo yaliyoadhirika na hali hiyo kwa vipindi tofauti ni pamoja na
Temeke, Kigamboni, Mbagala hadi Mkuranga na Chang'ombe baada ya gari
kugonga nguzo ya umeme katika eneo la Mkuranga na upepo mkali kuezua
bati kutoka kwenye jengo katika eneo la Shauri moyo na kulirusha juu ya
line ya umeme inayoanzia Ilala hadi Mkuranga.
Eneo
lingine ni Mandela Road hadi Tabata baada ya mvua na upepo kusababisha
wire kukatika katika kwa span mbili eneo la LandMark Hotel.
Eneo
lingine ni Kimara hadi Kibamba kutokana na Transformer iliyolipuka eneo
la Kimara na nguzo mbili za line kubwa zilizoanguka kutokana na mvua.
Eneo
la kati kati ya jiji lilipata hitilafu ya muda mfupi baada ya upepo
mkali kudondosha kamba inayotumika kwenye ujenzi kutoka jengo
linalojengwa karibu na yaliyokuwa makao makuu ya NMB na kudondoka kwenye
line ya umeme ya C8.
Wateja
wanaopatia umeme kutoka kituo cha Mbezi waliathirika na tatizo la Cable
ya 33kV na d.c supply kwenye kituo hicho. Maeneo ya Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam, Chuo kikuu cha Ardhi, Makongo, Mwenge na Changanyikeni
yaliathirika kwa muda.
Mafundi
wetu walifanya jitihada kubwa japo katika mazingira ya mvua kurekebisha
matatizo hayo katika muda mfupi kadiri ilivyowezekana.
Pamoja
na changamoto hii, tunapenda kuwahakikishia wateja wetu nchi nzima
kwamba hali ya umeme imeendelea kuimarika na umeme umekuwa ukipatikana
nchi nzima ukiacha hitilafu ndogo za hapa na pale za kiufundi.
Kulingana
na tahadhari zilizotangulia kutolewa na mamlaka ya hali ya hewa huenda
mvua hizi zilizoanza zikaendelea kwa muda mrefu hivyo tunawaomba
ushirikiano kutoka kwa wananchi katika kukabiliana na adhari kama hizi.
Tunawaomba radhi wateja wote walioathiriwa na hali hii.
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao
Post a Comment