Baadhi
ya mitambo katika Kituo cha Kupokelea Gesi Asilia kutoka Songosongo na
Mtwara kilichopo Somangafungu wilayani Kilwa Mkoani Lindi
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kulia) na
Naibu wake, Mhandisi Paul Masanja (kushoto) wakimsikiliza Meneja wa
Kampuni ya GASCO, Mhandisi Kapuulya Musomba (hayupo pichani) akiwaeleza
kuhusu Kituo cha Kupokelea Gesi cha Somangafungu. Katikati ni Msimamizi
wa Kituo hicho, Mhandisi Msafiri Peter.
Baadhi ya mitambo ya kupokelea gesi asilia iliyopo kwenye maeneo kilipo kisima cha gesi asilia cha Mnazi Bay Namba 3.
Sehemu
ya Mitambo ya kuchakata gesi asilia ya Madimba inavyoonekana wakati wa
usiku. Kituo hicho cha Madimba kilitembelewa na viongozi hao na kujionea
shughuli zinazoendelea kituoni hapo.
Sehemu
ya eneo lililokumbwa na Mmomoyoko wa ardhi uliotokea Mwezi Januari
mwaka huu katika kijiji cha Msimbati baada ya mvua kubwa iliyoambatana
na upepo mkali kunyesha katika maeneo hayo. Katika eneo hilo bomba kubwa
la gesi asilia linakatiza kuelekea kwenye kituo cha kuchakata gesi
asilia cha Madimba.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (wa sita
kutoka kushoto) na Naibu wake, Mhandisi Paul Masanja (kushoto kwake)
wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wengine mara baada ya
kutembelea kisima cha gesi asilia cha Mnazi Bay namba 3 (MB 3).
****
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo na Naibu
wake, Mhandisi Paul Masanja pamoja na Kamishna wa Nishati, Mhandisi
Hosea Mbise hapo jana walifanya ziara kwenye maeneo mbalimbali
yanayopitiwa na mradi mkubwa wa Gesi Asilia.
Lengo
kuu la ziara hiyo ni kujionea shughuli zinazoendelea kwenye mradi wa
gesi asilia pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa maeneo hayo kuhusu
masuala mbalimbali ya shughuli zao za kila siku.
Maeneo
ambayo yalitembelewa na viongozi hao ni pamoja na Kituo cha Kupokea
Gesi Asilia ya Mtwara na Lindi cha Somangafungu (Somangafungu Gas
Receiving Station) kilichopo wilayani Kilwa, mkoa wa Lindi; Visima vya
gesi asilia vya Mnazi Bay na Msimbati; Sehemu iliyoathiriwa na
Mmomonyoko wa ardhi ya Msimbati na Kituo cha Kuchakata gesi asilia cha
Madimba cha mkoani Mtwara.
Wengine
katika ziara hiyo ni Kamishna Msaidizi wa Nishati sehemu ya Gesi
Asilia, Mhandisi Norbert Kahyoza, Meneja wa Kampuni ya Gesi Asilia
(GASCO), Mhandisi Kapuulya Musomba na Maafisa kutoka Wizara ya Nishati
na Madini.
Ziara
hiyo ni miongoni mwa mikakati iliyowekwa na viongozi hao kukagua
shughuli mbalimbali za masuala ya Nishati na Madini kote nchini.
Post a Comment