Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchanguzi Jaji Msitafu Damian Lubuva akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya majina ya wabunge wa
Viti Maalum yatapatikana katika Vyama husika kwa mujibu wa Orodha
iliyowasilishwa Tume na kila Chama ila Tume (NEC)iweze kufanya Uteuzi,
kikao hicho kimefanyika leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Kaimu
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Emmanuel Kavishe.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Msitafu Damian Lubuva
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
TUME
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza Viti Maalum vya Wabunge 110 kwa
vyama vitatu ambavyo vimevuka asilimia tano ya kura za wabunge.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji
Mstaafu, Damian Lubuva amesema idadi ya wabunge imeongezeka kwa kufikia
asilimia 40 kutokana na uamuzi wa serikali wa mwaka 2010 kwa kuongeza
idadi ya viti maalum vya wanawake.
Lubuva
amesema kutokana na kuwepo majimbo ya nane ambayo hayakufanya
uchaguzi kunafanya viti vitatu kutokuwepo, baada ya uchaguzi wa majimbo
hayo viti vitarudi kwa vyama.
Katika
mgawanyo wa viti maalumu vya wanawake katika bunge linalotarajiwa
kuanza hivi karibuni Chama cha Mapinduzi (CCM), kimepata viti 64, Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) viti maalum 36 na Chama cha
Wananchi (CUF) Viti Maalum 10.
Majina
ya viti maalum yatapatikana katika vyama husika kwa mujibu wa orodha
iliyowasilishwa Tume ya kila chama ili tume iweze kufanya uteuzi.
Post a Comment