Wakazi
wa Kijiji cha Nyarugusu wilayani Geita wameandamana hadi katika
Zahanati ya kijijini hapo kwa madai ya Nesi kuhusika kusababisha kifo
cha mama mjamzito aliyekosa huduma kwa uzembe wa nesi wa zamu.
Inadaiwa
kuwa Novemba 18 Marehemu Kabula George alifikishwa katika Zahanati ya
Nyarugusu ambapo alipokelewa na Nesi wa Zamu majira ya saa tano usiku.
Nesi
huyo alimhudumia na kumwambia asubiri baada ya saa nne na nesi huyo
aliondoka na kwenda kulala ambapo Kabula alizidiwa na uchungu bila
msaada na hatimaye kufariki.
Majira
ya saa mbili baada ya wananchi kupata taarifa ya tukio lilomkuta
marehemu Kabula,waliandamana kituoni hapo na kuanza kurusha mawe
yalovunja baadhi ya madirisha.
Wananchi wamedai kuwa wamechoshwa na huduma zisizoridhisha na vitendo vya rushwa vilivyokithiri.
Wananchi hao wamedai ili kupata suluhisho la tatizo hilo lazima nesi huyo aondoke kituoni hapo
Tukilage Mhema Mganga Mfawithi Zahanati ya Nyarugusu amedai hana taarifa za malalamiko waliyoyatoa wananchi.
Wananchi wamegoma kwa maiti kutolewa bila ya manesi hao kuondoka katika kituo hicho.
Huduma zilisimama kwa zaidi ya saa nanae hali iliyopelekea baadhi ya wagonjwa kwenda kutafuta huduma sehemu nyingine.
Baadhi
ya viongozi ikiwemo jeshi la Polisi Wilaya lilifika na kukaa na uongozi
wa Hospitali na hatimaye kuja na muafaka ulioonekana kukubalika na
wananchi.
Kamanda
wa Polisi Wilaya ya Geita Ally Wendo amesihi wananchi kutokuvunjwa
sheria itakayosababisha vurugu zinazoweza kuleta madhara.
Hatimaye mwili wa Marehemu natolewa na kwenda nyumbani kwa taratibu za mazishi
Post a Comment