Mkuu
wa Wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akisalimiana na wananchi alipofanya
ziara katika hosptali teule ya Machame na kuzungumza na wafanyakazi.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akizungumza na wafanyakazi wa Hosptali teule ya Machame (hawapo pichani).
Mkurugenzi wa Hosptali hiyo,Dkt Saitore Laizer akizungumza katika kikao hicho.
Baadhi ya viongozi wa Hosptali hiyo na viongozi wa serikali wa wilaya ya Hai.
Baadhi ya wafanyakazi.
Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi katika hosptali ya Machame ,Dkt Fredrick Muro akizungumza katika kikao hicho.
Baadhi ya watumishi wa Hosptali hiyo.
Baadhi ya madktari wa hosptali teule ya Machame.
Mkuu wa wilaya akiondoka katika hosptali hyo mara baada ya kumalizika kwa kikao na watumishi.
******
Na Dixon Busagaga
Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
HALMASHAURI
ya wilaya ya Hai,mkoani Kilimanjaro, imewasimamisha kazi watumishi wake
wanne kwa tuhuma za kughushi hati za mishahara na kughushi nyaraka
zilizofanikisha kuchukua jumla ya kiasi cha sh Mil 73.4 zikiwemo fedha
za malipo ya muda wa kazi wa ziada kwa madaktari na wauguzi wa Hospitali
teule ya Machame.
Tuhuma
hizo pia zina mtaja Mweka hazina wa Hosptali hiyo anayedaiwa
kushirikiana na watumishi wa halmashauri hiyo kufanya ubadhirifu wa
fedha na kwamba tayari Uongozi wa hosptali hiyo iliyo chini ya Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Kaskazini ,umekwisha
mfukuza kazi.
Watumishi
wawili kati ya wanne wamesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbili
tofauti,moja ni kughushi hati za mishahara,vitambulisho na sahihi za
watumishi waliostaafu na wengine kuacha kazi na kuchukua mikopo wa Mil
35 katika benki ya CRDB kwa majina ya watumishi walioacha kazi.
Post a Comment