Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeendelea na zoezi la kuwaapisha wabunge wateule mbele ya Spika Job Ndugai.
Hiki ni kikao cha pili cha Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Zoezi la kuapishwa wabunge wateule limeanza majira ya saa tatu asubuhi baada ya kuahirishwa jana.
Baadhi
ya wabunge waliopata nafasi ya kuapishwa asubuhi ya leo wamekula kiapo
cha utii na uaminifu kuonyesha utayari wa kuwatumikia wananchi.
Bunge
limeahirishwa saa tano kamili asubuhi hadi saa 11 jioni ambapo
linaendelea na zoezi la kuwaapisha wabunge wateule waliobaki.
Post a Comment