Ujanja wa mjini! Jamaa
aliyejipachika cheo kuwa yeye ni Afisa Usalama wa Taifa, Ofisi ya Waziri
Mkuu akijitambulisha kwa jina moja la Manase amekiona cha moto baada ya
kunaswa na kufungwa kamba mwilini na mtu aliyesema ni daktari wa
Kliniki ya Head 2 ya jijini Dar, Fortdas Fidell.
Tukio hilo la aina yake
lilitokea Jumatano ya Februari 10, mwaka huu katika kliniki hiyo
inayojishughulisha na tiba ya mifupa na mazoezi iliyopo Mtaa wa Ununio,
Kata ya Kunduchi wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo risasi
sita zilipigwa hewani na mtu aitwaye Mashaka Ndonde ili kumdhibiti
mtuhumiwa huyo.
Post a Comment