Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

JESHI LA POLISI LAKAMATA MAJAMBAZI SABA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam imewakamata majambazi saba ndani ya wiki moja waliofanya matukio mbalimbali ya ujambazi Jijini humo.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam imewakamata majambazi saba ndani ya wiki moja waliofanya matukio mbalimbali ya ujambazi Jijini Dar es Salaam, wawili kati yao watuhumiwa hao wakiuwawa baada ya kushambuliwa na wananchi wenye hasira kali.

Akiongea leo jijini Dar es salaam Kamishna wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema kuwa katika oparesheni hiyo pia walifanikiwa kukamata lita 60 za Gongo, silaha aina ya SMG pamoja na bastola zilizokuwa zikitumiwa na majambazi, bangi kete 250, puli 110 pamoja na watuhumiwa wengine 130 kwa makosa mbalimbali.

Kamishna Sirro ameeleza pia kuwa wamefanikiwa kumkamata mwanamke mmoja anayetuhumiwa kwa makosa ya kuwaangalia wateja wanaotoka na fedha benki na kutoa taarifa ili wavamiwe na kunyanga'anywa fedha zao.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top