Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KESI YA KAFULILA YAPIGWA KALENDA


 Mlalamikaji wa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi ya ubunge jimbo la kigoma kusini David Kafulila akiongea na waandishi wa habari nje ya mahakama ya hakimu mfawidhi mkoa wa Kigoma baada ya Jaji kuhairisha kesi yake

  Wakili wa kafulila profesa safari akiongea na waandishi nje ya mahakama ya hakimu mfawidhi wa mkoa baada ya jaji kuhairisha kesi.
Baadhi ya wananchi wa mkoa wa kigoma wakiwa nje ya viunga vya mahakama ya hakimu mfawidhi wa mkoa kwaajili ya kusikiliza kesi ya David Kafulila wa NCCR Mageuzi ya kupinga matokeo ya ubunge dhidi ya Hasna Mwilima wa CCM


Na Editha Karlo wa blog ya jamii Kigoma

KESI No. 2 ya mwaka 2015 ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Kigoma kusini iliyofunguliwa na mlalamikaji  David Kafulila dhidi ya mbunge Hasna Mwilima,Msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria mkuu wa serikali imeahirishwa leo na mahakama kuu kanda ya Tabora mpaka  marchi 9, mwaka huu itakapoanza kusikilizwa tena.

Kesi hiyo ambayo ilikuwa  ianze mapema leo katika mahakama ya hakimu mkazi Kigoma,  Mbele ya Jaji Dr Wambari ambae pia ni Mkuu wa chuo cha sheria lushoto mkoani Tanga, imeahirishwa kwasababu mshatakiwa Hasna pamoja na wakili wake Kennedy Fungamtama pamoja na mawikili wa serikali kushindwa kufika mahakamani hapo, kwa madai ya kuchelewa kupata wito wa mahakama hyo, huku mlalamikaji David Kafulila akifika na wakili wake Prof Safari.

Katika mazingira hayo Jaji Wambari aliagiza mawasiliano yafanyike kwa pande hizo ili kujua ni lini kwa hakika mawakili hao wataweza kushiriki katika kesi hiyo.

Kutokufika kwa mlalamikiwa  na mawakili wake na wale wa upande wa serikali ilipelekea zoezi la kusikiliza kesi hiyo kusimama kwa saa mbili kutoka saa tano asubuhi  mpaka saa saba mchana na baada ya hapo hakimu mfawidhi wa Mkoa wa Kigoma kwa niaba ya Jaji silivesta Kahinda alisema  kuwa kesi itaendelea march 9 mwaka huu na kwamba kwakuwa tarehe hiyo imependekezwa na mawakili na pande zote mbili.

Akiongea na mtandao huu mlalamikaji wa kesi hiyo David Kafulila alusema luwa anakubiana na uamuzi wa mahakama hivyo aliwataka wananchi wawe na subiri hadi hiyi tarehe 9 march mwaka huu.

""Jaji mkuu na Jaji kiongozi wamekuwa dhamira  kwa sasa kuwa kesi za uchaguzi zimalizike haraka na hivyo kufikia tarehe hiyo ya march 9,  kesi inatarajiwa kusikilizwa mfululizo hadi itakafika
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top