Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KIPINDUPINDU CHAZIDI KUONGEZEKA


Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii,Jinsia,Wazee na watoto, Ummy Mwalimu akizugumza na wandishi wa habari juu ya takwimu za wiki iliyopita zinaonyesha kuwa kuanzia Februari  8 hadi 15 mwaka huu, idadi ya wagonjwa walioripotiwa wiki hii imeongezeka kutoka 242 ya wiki iliyoishia ya February 7 hadi imefikia wagonjwa  528 ambapo ni sawa na ongezeko la 118%, kati yao watu 5 walipoteza maisha.leo jijini Dar es Salaam,kusoto ni Katibu Mkuu wa Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii,Jinsia,Wazee na watoto,Dk.Mpoki Ulisubisya

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

UGONJWA wa kipindupindu hadi kufikia Februari 14 mwaka huu , jumla ya watu 15,853 wameugua ugonjwa huo, na kati yao watu 243 wamepoteza maisha. 

Akizungumza na waandishi wa Habari wa Jijini Dar es Salaam leo, Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii,Jinsia,Wazee na W    atoto, Ummy Mwalimu amesema takwimu za wiki iliyopita zinaonyesha kuwa kuanzia Februari  8 hadi 15 mwaka huu, idadi ya wagonjwa walioripotiwa wiki hii imeongezeka kutoka 242 ya wiki iliyoishia ya February 7 hadi imefikia wagonjwa  528 ambapo ni sawa naongezeko la 118%, kati yao watu 5 walipoteza maisha.

Amesema ongezeko hili limechangiwa zaidi na kuibuka tena kwa ugonjwa huu mkoani Iringa katika Halmashauri ya Iringa ambayo imeripoti jumla ya wagonjwa 199 kwa wiki iliyopita ikiwa ni sawa na 38% ya wagonjwa wote walioripotiwa kwa wiki husika.

Ummy amesema awali ya  Julai mwaka  jana , Mkoa wa Iringa uliwahi kuripoti wagonjwa 2 kwa siku moja tu, hata hivyo wagonjwa hao waliripotiwa katika halmashauri tofauti za Mufindi (1) na Iringa Mjini (1).

Amesema kwa Mkoa wa Dar Es Salaam ambapo ugonjwa ulidumu sana kwa muda wa miezi 4 na baadae kutoweka kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa umeanza tena kuripoti wagonjwa kwa  wiki iliyopita mkoani Dar es salaam waliripotiwa wagonjwa 6 ambao walitokea Manispaa ya Temeke.

Aidha amesema  mikoa ambayo imeripoti kuwa na wagonjwa kwa wiki iliyopita ni 11 ikiongozwa na Iringa 199 (Halmashauri ya Iringa Vijijini 199)  ikifuatiwa na Mkoa wa Mwanza 87 (Ilemela 31, Ukerewe 26, Nyamagana 15, Buchosya 11 na Sengerema 4), Mara 84 (Musoma mjini 36, Tarime vijijini 17, Musoma Vijijini 12, Butiama 10, Tarime Mjini 5 na Rorya 1). Mikoa mingine ni pamoja na Morogoro 54, Arusha 49, Simiyu 16, Dodoma 11, Mbeya 8, Kilimanjaro 8, Dar es salaam 6 na Manyara 6.


Wizara imekuwa ikikabiliana  na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na mwitikio mdogo wa jamii katika kudhibiti ugonjwa hasa kwenye suala la usafi wa mazingira na vyoo, pamoja utumiaji wa maji safi na salama. Hii ni pamoja na kufuata sheria ndogo ndogo zilizowekwa na jamii husika katika kuhakikisha suala zima la usafi.

Hata hivyo Ummy, amesema uelewa mdogo wa jamii kuhusu sababu zinazochangia kuwepo kwa ugonjwa wa kipindupindu pamoja na mila potofu zimekuwa ni changamoto katika swala zima la kumaliza ugonjwa huu, kama ilivyodhihirishwa huko Kyela mkoani Mbeya ambako mila potofu zimehusishwa na sababu za ugonjwa wa kipindupindu na kusababisha vifo kwa watu wasiokuwa na hatia.

Waziri huyo amesisitiza kuwa mikoa na halmashauri zote kutilia mkazo suala la uelimishaji jamii kwa kushirikisha viongozi mbalimbali ikiwa pamoja na ushirikishwaji wa walimu wa shule, viongozi wa dini, kimila  na viongozi wengine wanaokubalika na jamii husika katika kuelimisha na haswa swala la mila potofu.
  
Wizara imeendelea kuchukua hatua mbalimbali  za kudhibiti ugonjwa ikiwa ni  pamoja na kupeleka timu mbalimbali kutoka ngazi ya taifa katika mikoa ambayo bado kuna changamoto ikiwa ni pamoja na Morogoro, Simiyu, Mwanza, Mara, Mbeya na Manyara ili kuweza kushirikiana na mikoa hiyo katika kudhibiti Ugonjwa wa Kipindupindu.

Amesema kutokana na ongezeko la wagonjwa katika Halmashauri ya Iringa Wizara imetuma timu ya wataalamu kushirikiana na timu za mkoa na Halmashauri katika shughuli za kudhibiti ugonjwa huu.

Aidha Wizara ilikwishapeleka dawa na vifaa tiba na juhudi za kupata dawa na vifaa zaidi zinaendelea. Bado naendelea kusisitiza mapambano ya Kipindupindu yanahitaji ushirikishwaji wa ngazi zote mpaka katika ngazi ya kaya hivyo tukishirikiana kwa pamoja tutatokomeza Kipindupindu.

Amesema  kutokana na uzoefu kutoka mikoa ya Dar Es Salaam na Iringa kutoweka na kurudi tena kwa ugonjwa huu, na pia kutokana na ukweli kuwa ugonjwa upo pia katika nchi za jirani, Wizara inasisitiza Mikoa na Wilaya kuendelea kuimarisha mikakati ya kuzuia wa kipindupindu na kuifanya kuwa endelevu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top